KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, October 19, 2014

Ancelotti kukutana na Raheem Sterling Anfield huku akikanusha kumtaka ajiunge Real Madrid

Raheem Sterling anavutia Madrid licha ya Ancelotti kusema hana mpango naye
Mashabiki wa Liverpool angalau wameenza kupata kupumua baada ya meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti kusema kuwa kikosi chake hakimuhitaji Raheem Sterling.
Sterling bado hajasaini mkataba mpya na Anfield, huku uwezo wake mkubwa kwasasa ukizidi kuibua tetesi nyingi kuwa kigogo hicho cha Hispania kilikuwa kikimnyemelea winga huyo mwenye umri wa miaka 19.
Ancelotti pia amekanusha kuwa  kuna nia kutoka Bernabeu, wakati huu ambapo Mtaliano huyo anaamini kuwa Madrid ina washambuliaji wengi wa kushambulia tayari na kwamba hakuna haja ya kuongeza nguvu ya Sterling, licha ya uwezo wake mkubwa alionao.
Amenukuliwa akisema.
‘kufikiria juu ywa mshambuliaji mwingine kwa Real Madrid ni ngumu kabisa.Ni wazi kuwa Sterling siyo mpango wetu’ Amesema.
‘Sterling ni mchezaji mwenye ubora wa juu, sina shaka ni mshambuliaji mkiubwa Ulaya lakini tayari tuna vipaji zaidi hapa.’
Ancelotti atakuwa na fursa nyingine ya kumuona Sterling akifanya vitu vyake uwanja wa wakati Madrid watakapo elekea huko kuifuata Liverpool kwa mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya usiku wa jumatano.