KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, October 26, 2014

Mkenya ashinda mbio za Frankfurt

Mark Kiptoo ameimarisha ushindi wake katika mashindano ya mbio za Frankfurt mwaka huu baada ya kuibuka mshindi.
Kiptoo mbaye alimaliza katika nafasi ya pili mwaka uliopita aliwaongoza wanariadha wengine wa Kenya kushinda nafasi tatu bora katika mbio za wanaume.
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 38 ambaye alishinda medali ya shaba katika mbio za mita 5000 katika mashindano ya jumuiya ya madola ,alimaliza mbio hizo na saa 2,dakika 6 na sekunde 49,katika mbio za kusisimua ambazo ziliamuliwa ikiwa imesalia kilomita moja.
Mike Kigen alimaliza katika nafasi ya pili kwa saa 2 dakika 6 na sekunde 59 naye Gilbert Yegon akawa wa tatu kwa saa 2 dakika 7 na sekunde 8 baada ya bingwa mtetezi pia kutoka kenya kupoteza uongozi na kundi la kwanza katika kituo cha kilomita 30.

No comments:

Post a Comment