KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, October 17, 2014

Mshambuliaji aliyebaka na kwenda jela kwa miaka miwili na nusu Ched Evans atoka jela na kuzua mjadala mkubwa nchini England

Mshambuliaji wa Sheffield Ched Evans atoka jela
Evans (kulia) akiwa katia picha na familia yake
Nyota wa kimataifa wa Wales ambaye alikuwa akiichezea Sheffield United, ametumikia jela kwa miaka miwili na nusu kufuatia kubaka msichana mwenye umri wa miaka 19

Nyota Evans akikutana na mpenzi wake Natasha Massey
 
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Sheffield United na timu ya taifa ya Wales Ched Evans ametoka jela Ijumaa ya leo baada ya kutumikia gerezani kwa nusu ya miaka mitano kufuatia kubaka.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye aliwahi kuichezea Manchester City alihukumiwa kwenda jela baada ya kupatikana na hati ya kumbaka mwanamke kwenye umri wa miaka 19 katika chumba cha hoteli.
Evans, ambaye aliondoka katika jela ya Wymott Prison karibu na Leyland kaskazini magharibi ya nchi ya England mapema hii leo ameahidi kuwa mtu mwema uraiani kuanzia hivi sasa.
Meneja wa Sheffield United Nigel Clough amekuwa akifikiria kama kuna uwezekano wa kumrejesha kundini lakini akikabiliwa na upinzani kutoka kwa watu zaidi ya 145,000 waliosaini kitabu maalumu kupinga kurejea klabu hapo kwa Blades.
Hapo jana naibu waziri mkuu wa Uingereza na mbunge wa Sheffield Nick Clegg waliitaka klabu hiyo kufikiria kwa makini kabla ya kuamua kumruhusu Evans kuichezea tena klabu yao.