KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, August 11, 2010

ASTON VILLA NEWS

Mmilikiwa wa klabu ya Aston Villa Randy Lerner amesema ni hivi punde tu atazungumzia juu ya kuondoka kwa aliyekuwa meneja wa klabu hiyo Martin O'Neill na jinsi ya kuyifanya klabu hiyo kusonga mbele.
Anasema ina eleweka kuwa O'Neill ameondoka katika klabu hiyo baada ya miaka minne ya kuitumikia klabu hiyo kwasababu hakupewa guarantee ya pesa zote za mauzo ya James Milner ambaye alikuwa katika mipango ya kuelekea Manchester ili afanikishe mipango ya usajili kwa wachezaji wapya.
Lerner ametanabaisha kuwa mwishoni mwa msimu uliopita aliweka wazi nia ya sera ya mauzo na kununua ('sell-to-buy' policy) baada ya kumfuatilia O'Neill katika kipindi cha misimu mitatu iliyotangulia lakini hata hivyo mmiliki huyo raia wa Marekani amesema hakukuwa na mabadiliko katika kuelekea kujenga klabu hiyo na kuwa ya kiushindani.
Lerner amesisitiza kuwa mipango ya kipaumbele ni kuingilia kati mipango ya uhamisho ya Milner na kutoa msaada kwa Kevin MacDonald ambaye amepewa dhamana ya kushika umeneja wa muda.

No comments:

Post a Comment