TRANSFER NEWS
Diego aelekea kukamilisha kuelekea Wolfsburg
Wolfsburg imekubali euro milioni €16 kama ada ya kiungo wa Juventus Diego.
Diego mwenye umri wa miaka 25 anaelekea kuwa ni nyota katika ligi ya kandanda nchini ujerumani maarufu kama Bundesliga.
Wolfsburg na Juve inasemekana walikuwa katika mazungumzo tangu jumatatu na imearifiwa kuwa mchezaji mwenyewe ndiye ambaye yupo katika mjadala wa maslahi yake “personal terms”.
Wakala wa wachezaji anayetambulia na FIFA Giacomo Petralito amekuwa katikati katika mipango ya uhamisho wa nyota huyo na ametanabaisha kuwa mambo yatamalizika hivi punde.
Juventus inajaribu kuimarisha kikosi chake baada ya kuwa katika msimu mbaya msimu uliopita kwa kumaliza katika nafasi ya saba katika ligi ya italia maarufu kama Serie A na taarifa zikiarifu wapo pia katika mpango wa kutafuta pesa kumnasa Michel Bastos wa Lyon ya ufaransa.
No comments:
Post a Comment