KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, August 6, 2010

Jan paulsen anawasubiri Nizar khalfan na henry Joseph

Ikiwa ni siku chache mara baada ya kutangaza kikosi chake cha kuanzia kazi ya kuifundisha timu ya taifa ya tanzania taifa stars, kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya Tanzania Joe paulsen amesema anawasubiri kwa hamu kubwa wachezaji wa tanzania wa kimataifa wanaochezea soka nje ya nchi ili kuweza kujumuika na wenzao wanaochezea soka nchini katika kukiandaa kikosi chake tayari kwa mchezo wake wa kwanza wa kujipima nguvu dhidi ya timu ya taifa ya Kenya Hrambee Stars mchezo ambao umepangwa kufanyika tarehe 11/august katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.akizungumza na blog hii Paulsen amesema anamatumaini makubwa kuwa viwango vya wachezaji hao vitakuwa katika hali nzuri kwa kuwa bado wanaendelea na ligi na kwamba uwepo wao utakuwa ni chachu ya kufanya vizuri katika mtihani wake wa kwanza kuifundisha Taifa Stars.

kwa upande wake kiungo Nizar Khalfan amesema anajisikia vizuri kuitwa katika kikosi hicho tayari kumenyana na Harambee Stars jumatano ijayo isipokuwa kinachosubiriwa ni kupata ruhusa kutoka kwa kocha wake wa Whitechaps ili ajiunge na wenzake kambini.
Nizar anasema ni faraja kocha mpya kuona mapema umuhimu wao walioko nje ya nchi na kwamba hiyo itakuwa ni changamoto mpya toka kwa kocha huyo.
Mchezaji mwingine aliyeitwa na kocha paulsen ni nahodha wa zamani wa Stars Henry Joseph ambaye naye anatarajiwa kuwasili wakati wowote kujiunga na wenzao ambao wameshaanza kambi mapema wiki hii.
Tangu kuwasili kwa Paulsen maswali yamekuwa ni juu ya uwezo wake wakufundisha na ni namna gani ataleta mabadiliko katika kandanda la Tanzania ambalo katika kipindi cha miaka minne iliyopita lilikuwa chini ya Mbrazil Marcio Maximo ambaye mkataba wake ulimalizika mapema mwezi june.Stars itakumbana na Harambee Stars ya Kenya ikiwa na nyongeza ya wachezaji wawili waliokuwa na matatizo na kocha Maximo kutokana na kile kilichoelezewa kuwa ni ukosefu wa nidhamu,wachezaji hao ni kiungo Athumani Iddi Chuji na mlinda mlango Juma Kaseja.

No comments:

Post a Comment