KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, August 5, 2010

TANZANIA NA NDOTO ZA SOKA BAADA YA MAXIMO
Joe paulsen
Baada ya kutajwa kumrithi kocha raia wa Brazil Marcio Maximo ambaye muda wakw wa kuitumikia Tanzania kama kocha mkuu wa nchi hii,watanzania wengi walitaka kujua huyu mtaalam mpya raia wa Dernmark ana sifa zipi ,ataifanyia nini Tanzania ,ataifikisha wapi Tanzania, je? hamu ya watanzania kuona ndoto zao za kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa kuanzia zitatimia kabla ya kuona Tanzania inafuzu katika fainali za kombe la dunia jambo ambalo linatazwa kama ndoto za mchana.
Macho ya watanzania sasa ni kwa kocha huyo Jan Paulsen mwenye umri wa miaka 64 ambaye kama sifa za kuifundisha timu ya taifa kwa kutegemeana na vigezo vya shirikisho la kandanda Tanzania (TFF) anavyo.
Mkataba wake ni wa miaka miwili kama ilivyokuwa kwa Maxomo hapo awali kabla ya kupata nyongeza ya mwaka mmoja kwa vipindi viwili na kufanya idadi ya miaka kuwa minne.
Waswahili wana msemo subira yavuta kheri,alisubiriwa maximo kwa miaka minne na hatimaye ikamalizika na ile kiu ya watanzania kuona ndoto zao angalau ya kushiriki tena fainali za mataifa ya Afrika tangu kufanya hivyo kwa mra ya mwisho ikayeyuka mwaka 1980 ikayeyuka.

Yanaandikwa mengi,yanasemwa mengi na yataendelea kusemwa mengi baada ya kuwasili kwa mdenish huyo, lakini ukweli utabaki palepale ni kwa Tanzania kushiriki fainali za mataifa ya Afrika na ikiwezekana kuona inacheza kombe la dunia.
Nguvu ya uwekezaji katika miaka mitano iliyopita ya mheshimiwa mpenda michezo Rais Jakaya Kikwete imekwenda akiwa na ndoto ya kuona michezo inasogea pahala ambapo wanajisifu mbele ya mataifa mengine itategemea na mabadiliko ndani ya kipindi chake cha miaka mitano ijayo maana ndiyo muda wake wa mwisho wa kuwepo madarakani kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kama mungu atamjalia kurejea madarakani baada ya uchaguzi wa mwezi Oktoba,hicho ni kipindi ambacho kocha mpya atakuwa katika mkataba wake.Sasa swali hapa ikashindikana hilo ndani ya muda huu Rais ajaye ataona michezo na hasa mpira wa miguu una maana kama si ni kupoteza muda na nguvu kubwa ya kiuchumi katika kitu ambacho hakiwezekani,sijui tuone mdenish atatufikisha wapi.


Amewahi kuchezea klabu ya Boldklubben Frem ya Dernmark na kufanya kazi ya kufundisha soka sehemu mbalimbali uzoefu wake utatusaidia ? na je ana mafanikio huko alikotoka ama anaanzia hapa Tanzania ? tusubiri tuone.
Tayari ametangaza kikosi chake cha kwanza cha wachezaji wake wa kuanzia huku akili ya kukiunda kikosi hicho na ufundi aliotumia umepongezwa kwa kuwa hakuwahi kuwajua wachezaji wa kitanzania huko nyuma,amekitaja kikosi kilicho cheza na timu ya taifa ya Brazil mwezi May na kuwaita wale walioitwa watovu wa nidhamu chini ya Marcio Maximo hawa ni mlinda mlango Juma Kaseja na Athumani Iddi Chuji.
Kikosi kamili ni walinda milango Jackson Chove(Azam), Shaabani Kado (Mtibwa) and Juma Kaseja (Simba) – walinzi wa pembeni ni Shadrack Nsajigwa (Yanga), Salum Kanoni (Simba), Juma Jabu (Simba), Stephan Mwasika (Yanga) na Idrissa Rajabu (Sofapaka, Kenya).

Walinzi wa kati ni Nadir Haroub(Yanga), Kelvin Yondani (Simba), Agrey Morris(Azam) na Erasto Nyoni (Azam).
Viungo ni Abdulhalim Humoud (Simba), Nurdin Bakari (Yanga), Henry Joseph (Kongsvinger, Norway), Athumani Idd (Yanga), Nizar Khalfani (Vancouver Whitecaps, Canada), Jabir Aziz(Azam Fc), Kigi Makasy (Yanga), Abdi Kassim (Yanga), Uhuru Selemani (Simba) na Selemani Kassim (Azam Fc).
Washambuliaji ni Mrisho Ngassa(Azam), John Bocco (Azam), Mussa Mgosi(Simba), Jerson Tegete (Yanga) na Danny Mrwanda (DT Long An Vietnam).
TFF inasema Jumla ya makocha 60 toka sehemu mbalimbali duniani kote waliomba nafasi hiyo ya kumrithi Maximo.
Lakini kulingana na matakwa ya Tanzania Paulsen akashinda kwa nini vigezo.
Huu ni uzoefu wake, baada ya kuachana na kucheza soka alirejea katika klabu aliyoichezea katika miaka ya 1980 klabu ya Boldklubben kabla ya kuelekea kuifundisha timu ya Koge Boldklub.

Mwaka 1990 aliitwa kama kocha msaidizi wa kocha wa wakati huo wa Dernmark Richard Moller Nielsen na alikuwa ni sehemu ya timu ya taifa ya nchi hiyo iliyoshinda michuano ya Euro ya mwaka 1992.
Baada ya kutwaa taji hilo la 1992, alipendekezwa kuwa kocha mkuu wa wa timu ya taifa ya nchi hiyo chini ya miaka 21 ameishikilia nafasi hiyo mpaka mwaka 1999 alipoteuliwa kuwa mkurugenzi wa michezo wa timu ya taifa ya taifa ya Singapore.
Wakati Vincent Subramaniam alipofukuzwa kazi mwaka 2001 kufuatia matokeo mabaya , Paulsen akachukua nafasi yake .hiyo haikuwa dawa kwa taifa hilo la Singapore na Poulsen akafukuzwa kazi mwaka 2002.
Alirejea Denmark kufanya kazi ya ukocha katika vilabu vidogo vidogo ndani ya nchi hiyo .mwaka 2006 alifikia makubaliano na Greve Fodbold kuwa kocha mpya lakini akapata ofa ya kazi nyingine kuifundisha timu ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 ya Jordan.
Mwishowe alifanya kazi hiyo katika klabu ya Jordan kwa miaka miwili na baadaye kupata kazi ya kuifundisha timu ya taifa ya Armenia.
Mwishoni mwa Mwezi 2009, Poulsen akaachana na kazi hiyo na mwezi june kupewa kazi na shirikisho la kandanda la Tanzania ,hii ni mara yake ya kwanza kufanya kazi barani Afrika hususan na Tanzania .
Poulsen amewasili Tanzania jumamosi ya tarehe 31 Julay 2010 usiku na siku iliyofuata akaanza kazi ya kuchagua kikosi cha timu ya taifa “taifa stars” kwa kushirikiana na makocha wa kizalendo na kamati ya ufundi ya shirikisho la kandanda la Tanzania (TFF).
Anasema malengo yake ni Taifa Stars inafuzu katika fainali za mataifa ya Afrika kutokea katika kundi D ikiwa na mataifa ya Algeria, Morocco na jamhuri ya kati(Central Africa Republic).

No comments:

Post a Comment