Sir Alex Furguson akiwa na mtendaji mkuu wa United David Gill |
Manchester
United imetangaza kutaka kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Barcelona mchezo
wa maandalizi ya kuanza msimu mpya wa ligi “pre-season” mjini Gothenburg chini Sweden.
Mchezo huu umepangwa
kufanyika jumatano August 8 uwanja wa Ullevi ambao ulitumika katika mchezo wa
fainali ya UEFA 2004.
Mtendaji mkuu
wa United David Gill amekaririwa kupitia mtandao wa klabu hiyo akisema
"mchezo
baina ya Manchester United dhidi ya Barcelona ni mchezo mkubwa katika soka
duniani hivyo tunajisikia faraja kufanya kazi na GotEvent kufanikisha mchezo
huu katika mji mzuri kama Gothenburg.
"tuna
mashabiki wetu wengi katika ukanda wa nchi za Scandinavia na ni mchezo ambao utakuwa katika
sehemu ya kujiandaa kwa msimu mpya."
Mara ya
mwisho kwa timu hizo kukutana ilikuwa July 30 2011 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika
FedEx field jijini Washington nchini Marekani na United ikashinda kwa mabao 2-1
mabao yakifungwa na Michael Owen.
No comments:
Post a Comment