KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, July 16, 2012

Dimitar Berbatov:Bora niondoke Manchester United

Dimitar Berbatov
Mshambuliaji wa Manchester United  Dimitar Berbatov ametoa kauli akisema ni bora kuondoka katika klabu hiyo.
Berbatov ambaye ameitumikia klabu hiyo michezo 21 tu amekuwa si chaguo tena la meneja wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson.
Sasa raia huyo wa Bulgaria ambaye alinunuliwa kwa gharama ya pauni milioni £30.75 mwaka 2008 anasema ni bora aondoke akatafute timu ambayo atakuwa na uhakika wa kucheza katika kikosi cha kwanza.
"naipenda hii klabu , lakini ni wazi kuwa haifai kwa mtu yoyote kama hupati nafasi ya kucheza," Berbatov amekaririwa kupitia mtandao wake. 
 “nataka kucheza ,nataka kutoa huduma lakini bila ya sababu ya kueleweka hilo halitokei hivyo kwa yoyote ni inakuwa bora kusema goodbye.”
Berbatov aliifungia United jumla ya mabao 14 katika msimu wake wa kwanza akitokea Tottenham alikuwa pia katika mchezo wa fainali wa Champions League ambapo walichapwa na Barcelona.

No comments:

Post a Comment