KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, July 16, 2012

Chelsea kuweka 'record' uhamisho wa Oscar


Chelsea inaimani kuwa wako katika uongozi wa mbio za kupata saini ya kiungo Oscar ambaye alihusishwa kutaka kuelekea Tottenham na Inter Milan.
Internacional imedai kuwa mwishoni mwa juma ilifikia katika hatua nzuri na Chelsea, lakini bado offer haijatolewa kwa ajili ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20.
lakini kwa mujibu wa taarifa zilizo zagaa huko Brazil ni kwamba The Blues huenda wakatoa offer ambayo itakuwa ya rekodi kwa Mbrazil huyo.
Akizungumza na Radio Gaucha rais wa Internacional Giovanni Luig amesema
"nataka uhamisho wa Oscar uwe mkubwa katika soka la  Brazil , na Offer ya Chelsea haiku mbali na hap."
Oscar ambaye amechezea michezo sita katika kikosi cha timu ya taifa anatarajiwa kuonekana katika michezo ya Olympic kule London.

No comments:

Post a Comment