Mashabaka wa kandanda nchini China wamkaribisha
Didier Drogba Shanghai
Nyota wa
kimataifa wa Ivory Coast Didier Drogba amewasili nchini China na akipokewa kwa
furaha na mashabiki wa kandanda nchini humo kwa ajili ya kuingia mkataba na
klabu ya Shanghai Shenhua.
Mashabiki
mamia kwa maelfu wa timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya soka wa klabu hiyo
inayoshiriki ligi kuu ya China wamempokea mshambuliaji huyo mwenye umri wa
miaka 34 kwenurv uwanja wa ndege wa Shanghai Pudong airport.
Drogba
imeripotiwa kuwa atakuwa akipokea mshahara wa dolari za kimarekani $300,000
(£193,000) kwa wiki na kumfanya kuwa ni mmoja wa wachezaji soka wanaolipwa pesa
nyingi duniani.
Drogba ni
miongoni mwa wachezaji wengi wa kigeni ambao wameelekea nchini China.
Anajiunga na
Nicolas Anelka katika klabu ya Shanghai Shenhua.
Baada ya
kuwasili akiongea Drogba amesisitiza
kuwa hakwenda huko kwa ajili ya pesa.
Amesema
"ingekuwa
rahisi kwake kuendelea kusalia ulaya , lakini nimechagua China. Pesa si kitu
muhimu sana nipo hapa kwa ajili ya kusambaza uzoefu wangu."
Mamia ya
mashabiki wamempokea Drogba katika uwanja wa ndege wa Shanghai wa Pudong hii
leo.
No comments:
Post a Comment