KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, July 22, 2012

Maradona: Cristiano Ronaldo hamfikii Messil


Diego Maradona amepaza sauti yake akitoa maoni yake kuwa mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo hataweza kufikia kiwango alicho nacho mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi.
Washambuliaji wote wawili wanaonekana kuwa katika nafasi sawa ya kushinda tuzo ya FIFA ya Ballon d'Orbaada ya kuwa na msimu mzuri lakini bado Maradona anadhani Mreno hamkaribii kabisa kiuwezo Muajentina.
Amenukuliwa akisema
"Cristiano Ronaldo hawezi kuwa katika kiwango kama alichonacho Messi. Lionel haitaji nguvu za kupiga alizonazo Cristiano Ronaldo. Messi yeye ana dribble yaani anakokota mpira kuelekea golini akiwa na mpira wake mguuni," Maradona alikuwa akiongea na  TVR.
Katika hatua nyingine muwasisi huyo wa jezi No.10 duniani alikuwa na maoni tofauti juu ya michuano ya ulaya ambapo aliandika juu ya Ronaldo ambapo alinukuliwa akisema Ronaldo ni mchezaji bora kama ilivyo kwa Lionel Messi, akichanganywa na aina ya uchezaji wake alipokuwa akiitumikia Ureno katika michuano hiyo
Katika hatua nyingine nyota huyo wa michuano ya kombe la dunia 1986 alichukizwa na kulinganishwa na  Messi.
Amenukuliwa akisema
"sipendi kulinganishwa naye .lakini kunilinganisha naye ni kitu kizuri sisi wote tunatumia miguu ya kushoto,wote tuna toka Argentine na tunang’ara"


No comments:

Post a Comment