Kiungo wa Arsenal
Aaron Ramsey bado ana matumaini kwamba nahodha wake Robin van Persie ataendelea kuwepo Emirates
Stadium baada ya msimu wa uhamisho kumalizika.
Kumekuwepo na
fununu juu ya hatma ya mduchi huyo tangu
alipotangaza kuwa hana mpango wa kujisajili tena na washika mitutu hao huku
akikosoa sera za usajili za klabu hiyo na mwelekeo wa klabu hiyo.
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 28 aliifungia Arsenal jumla ya magoli 30 msimu
uliopita na kuipa nafasi kikosi cha meneja Arsene Wenger kushika nafasi ya tatu
katika ligi kuu ya nchini Uingereza.
Kiungo Ramsey
ambaye kwasasa anajiwinda na Olympics akiwa katika kikosi cha Great Britain
anafikiri kuwa itakuwa kupata mtu muafaka atakaye weza kufunga magoli hayo ya
Van Persie endapo ataondoka.
Akoongea na Belfast
Telegraph amenukuliwa akisema
"hatujui
nini kinaendelea lakini tuna matuini kuwa atakuwepo Arsenal.
"alikuwa
na msimu mzuri msimu uliopita na ni mchezaji mkubwa kwetu hivyo tuna matumaini
atasalia."
Arsenal
tayari imewasajili washambuliaji Lukas Podolski na Olivier Giroud pengine ni
kutokana na kile kinachoonekana kutaka kuondoka kwa Van Persie.
Kuanza vibaya
kwa msimu kwa klabu hiyo kunaonekana pengine kulisababishwa na Wenger kuacha
kufanya usajili wakueleweka mapaka dakika ya mwisho wa uhamisho unamalizika.
Ramsey anaamini
kuwa endapo biashara ingekwenda vizuri tangu mapema basi pengine wangeanza
msimu vizuri kampeni yao nap engine kupunguza pengo kubwa la points 19 kati yao
na wale waliokamata nafasi ya pili Manchester United.
No comments:
Post a Comment