Diego Maradona |
Mwasisi wa
soka la Argentina Diego Maradona anaamini na kupigilia msumari kuwa timu ya
taifa ya Hispania ya sasa haifungiki na ni timu kihistoria.
Maneno yake
yanakuja baada ya kisago cha haja kwa timu ya taifa ya Italia cha mabao 4-0 chini
ya Vicente del Bosque katika mchezo wa fainali ya mataifa ya Ulaya 2012.
Huo ulikuwa
ni ushindi ambao ulitengeneza rekodi kwa Hispania kushinda mataji matatu
makubwa duniani mfulilizo ikiwa ni mara ya kwanza kutokea duniani timu ya taifa
kupata mafanikio makubwa kiasi hicho.
Maradona
ambaye kwasasa ni meneja wa klabu ya Al Wasl ya Dubai anaamini La Roja ilistahili
ubingwa huo kufuatia kutawala michezo karibu yote iliyocheza katika fainaali za
majira haya ya kiangazi katika miji ya Poland na Ukraine.
Katika ukurasa
wake katika gazeti la ‘Times of India’ Maradona ameandika
“[Spain] imedhihirisha
wazi kuwa si tu timu bora ya taifa duniani lakini pia ni bora katika kucheza
soka dunaini.
“hakuna
wakuifunga ‘Spanish machine’. Cristiano Ronaldo alijaribu akiwa na Ureno lakini
Hispania ilimdhibiti.
“[Andrea]
Pirlo alijaribu na Hispania ilimdhibiti kwa kutumia wachezaji wanne
waliomzunguka”
No comments:
Post a Comment