Mshambuliaji
wa Manchester City Carlos Tevez ameendelea
kusalia katika mawindo ya AC Milan hii ikiwa ni kwa mujibu wa wakala wake
ambayo amekuwa akihusika na mpango huo.
Tevez amekuwa
akihusishwa na kutaka kuelekeea Serie A mara kadhaa wakati ambapo kumbukumbu ya
kuelekea Milan mwezi January ikionyesha
mpango huo kuvunjika katika dakika za mwisho kutokana na mpango wa kuuzwa kwa Alexandre
Pato kwenda Paris Saint-Germain kuharibika.
hata hivyo
mpango unaarifiwa kurejea kufuatia kuwepo na taarifa kuwa Zlatan Ibrahimovic ataondoka
San Siro kwenda PSG.
No comments:
Post a Comment