Wayne Rooney
amethibitshwa kuwa nahodha wa England katika mchezo wa ijumaa kuwania kufuzu
kombe la dunia dhidi ya San Marino mchezo utakao chezwa katika dimba la Wembley
Stadium.
Kocha wa
timu ya taifa ya England Roy Hodson pamoja na chama cha soka nchini humo
wamesema nyota huyo wa Manchester United ataongoza kikosi cha simba watatu
kufuatia kukosekana kwa nahodha ‘skipper’ Steven Gerrard ambaye ana adhabu ya
kusimama mchezo mmoja iliyotokana na mchezo dhidi ya Ukraine lakini pia nahodha
msaidizi Frank Lampard akisumbuliwa na matatizo ya paja aliyoyapata katika
mchezo wa Chelsea dhidi ya Norwich City jumamosi.
Akinukuliwa katika
mkutano na waandishi wa habati Rooney amesema
"ni
heshima kubwa, ni kitu ambacho kiukweli najivunia na ni changamoto kubwa kwangu
mbali na ukweli kwamba ni kitu nakitaka katika siku zijazo. Naamini tuataibuka
na ushindi"
Akielezea juu
ya maamuzi hayo Hodgson amesema,
"ninafuraha
kwa kuwa Rooney atapatikana katika mchezo huo. Nafurahia kufanya kazi na Wayne,
tumekuwa na mashindano mazuri ya Ulaya na Rooney, nilihuzunika alipokosekana
katika michezo ya mwezi September lakini nafurahia amerejea "
Ni miaka
mitatu imepita tangu Rooney kuongoza kikosi cha England ambapo mara ya mwisho
kufanya hivyo ilikuwa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Brazil mjini Doha November,
2009, ambapo katika mchezo huo simba watatu walipoteza kwa kufungwa bao 1-0.
JUAN MATA AMSIKITISHA TORRES
Fernando
Torres ametanabaisha kuwa Juan Mata amekuwa si mtu mwenye furaha kufuatia kuachwa
katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania.
Nyata huyo
wa zamani wa Valencia amekuwa katika
kiwango safi akiwa na timu yake ya Chelsea msimu huu, huku Torres akiamini Mata
ni mchezaji muhimu katika kikosi cha Hispania ‘La Roja boss’ cha kocha Vicente del Bosque.
Amenukuliwa Torres
akisema
"Mata hana
raha baada ya kuachwa katika timu ya taifa lakini anacheza vizuri. Siwezi kusema
sana kuhusu yeye kwasababu sitaki kuonekana namsemea "
Torres pia
amesisitiza kuwa mabingwa hao wa dunia na Ulaya watakuwa na kazi kubwa katika mchezo
wa group I dhidi ya France mchezo utakao
pigwa jumanne lakini pia wakiwa katika maandalizi ya mchezo wao wa Ijumaa dhidi
ya Belarus.
No comments:
Post a Comment