Simba asiyefugika
atakosekana kwa mara ya pili mfululizo katika fainali ya mataifa ya Afrika
wakati mataifa kadhaa yakielekea Afrika kusini.
Cameroon
ilitakiwa kushinda si chini ya mabao 2-0 kwa kuzingatia matokeo ya mchezo wa mkondo
wa kwanza ambapo walifungwa na Cape Verde lakini licha ya Samuel Eto'o kurejea
katika kikosi cha timu hiyo bado ushindi ulishindikana zaidi ya kuishia kupata matokeo
ya ushindi wa mabao 2-1 na hivyo kushindwa kufikia dhamira.
Licha ya
kuondoshwa mashindanoni bado mashabiki wa soka wa Cameroon walishangilia bao
zuri la mchezaji kinda mwenye umri wa miaka 16 ambaye ndio kwanza alikuwa
akianza kuitumikia timu ya taifa ya Cameroon Fabrice Olinga, akiwa ni mchezaji zao la
taasisi ya Samuel Eto'o Foundation, shambulizi lake lilitokana na akili yake.
Mataifa yaliyofuzu
ni pamoja na South Africa, Zambia, DR Congo, Ethiopia, Nigeria, Niger, Ghana,
Mali, Togo, Burkina Faso, Angola, Cape Verde, Algeria, Morocco na Tunisia.
Ethiopia imefuzu
kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1982, baada ya kuwachapa Sudan 2-0 na hivyo
kufuzu kutokana na faida ya bao la ugenini wakati ambapo Niger ikifuzu baada ya
kuwafunga Guinea kwa mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa mjini Niamey.
Burkina Faso
walihitaji goli la dakika za mwisho kupitia kwa Alain Traore na hivyo
kujihakikishia ushindi wa mabao 3-1dhidi ya Jamhuri ya kati ili kukwepa kichapo
cha faida ya goli la ugenini.
Emmanuel
Adebayor alifunga goli muhimu lililo amua hatma ya Togo baada ya kuichapa Gabon
3-2, wakati ambapo mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Manucho alipoibuka shujaa wa Angola akifunga
magoli mawili na kuwadhoofisha Zimbabwe kwa mabao 2-0.
DR Congo imefungwa
mabao 2-1 na Equatorial Guinea lakini imefanikiwa kufuzu kwa ushindi wa jumla
wa mabao 5-2, wakati ambapo Algeria ikiwachapa Libya 2-0 na kujihakikishia ushindi wa jumla
wa mabao 3-0.
Ghana, Mali,
Morocco, Nigeria, Tunisia na bingwa mtetezi Zambia, wao wamefanikiwa kufuzu
katika michezo yao iliyochezwa jumamosi.
Cote
d'Ivoire ni kama itaungana na mataifa mengine yaliyofuzu kufuatia mchezo wao
dhidi ya Senegal kuvunjika baada ya kutokea kuvurugu za mashabiki licha ya
kwamba shirikisho la soka barani Afrika kuwa kimya kufuatia tukio hilo
lililotokea katika mji wa Dakar nchini Senegal.
No comments:
Post a Comment