Meneja wa
timu ya taifa ya Senegal Ferdinand Coly amesema wanatarajia kuwa katika kipindi
kigumu mbeleni, baada ya vurugu zilizo sababishwa na mashabiki wa soka wa nchi
yao kiasi kupelekea mchezo wa kuwania kufuzu fainali za maraifa ya Afrika dhidi
ya Ivory Coast kuvunjika jumamosi.
Vurugu hizo
zilitokea wakati ambapoa Ivory Coast ikiongoza kwa mabao 2-0 ambayo yalikuwa ni
matokeo ya jumla ya mabao 6-2.
Amenukuliwa Coly
akisema
"tunaelekea
katika wakati mgumu lakini Senegal itakubaliana na adhabu".
"kwa
wachezaji imewaumiza sana hususani wachezaji wachanga"
Mashabiki wa
Senegal walianza kuwasha moto majukwaani na kutupa vitu uwanjani zikiwa
zimesalia dakika 15 mchezo huo kumalizika mjini Dakar, muda mfupi baada ya
mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba kukandamiza bao la pili kwa
njia ya penati.
No comments:
Post a Comment