Chama cha
soka ncini England FA kimethibitisha kuwa wachezaji wawili wa Chelsea Frank
Lampard na Ryan Bertrand hawatakuwemp katika kikosi cha nchi hiyo katika mchezo
wa kuwania nafasi ya kushiriki fainali ya kombe la dunia 2014 dhidi ya Poland mchezo
ambao unatarajiwa kuchezwa jumann e kutokana na kusumbuliwa na majeraha na
kuumwa.
Taarifa ya
FA imenukuliwa ikisema,
"Frank
Lampard na Ryan Bertrand wameondolewa katika kikosi cha England kwa ajili ya
mchezo wa kuwani kufuzu kombe la dunia dhidi ya Poland,"
"Lampard
ana matatizo ya msuli na Bertrand ni mgonjwa ndio maana hawakuwepo katika
kikosi kilichopata ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya San Marino, na pia
hawatakuwepo katika mchezo wa jumanne"
Meneja Roy
Hodgson hapo kabla alikuwa akimtegemea Lampard kwamba huenda kapata nafuu na
kuwepo katika mchezo huo utakao pigwa kule Warsaw.
Xavi amsifia Messi kwa kusema hakuna
kama Messi
Nyota wa Barcelona
Xavi amemsifia nyota mwenzake katika timu yake ya Barcelona Lionel Messi, kwa kusema hakuna
kama yeye, akiwazodoa wanao mfananisha na Cristiano Ronaldo lakini pia akimpa
heshima kocha wake Tito Vilanova, kwa kusema ana mambo mengi yanayo fanana na
mtangulizi wake Pep Guardiola.
Amenukuliwa na
rediao Catalunya akisema,
"ndani ya
chumba cha kubadilishia nguo, ‘Leo’ Messi ni mtu mmoja mkimya sana. Ni mtu wa
kipekee"
"ni
namba moja kwa upande wangu hakuna mwingine. Kwa kusema haki ni bora kabisa, na
mchezo wake ni muhimu na bora kuliko Cristiano [Ronaldo]."
Xavi na Messi
wamekuwa msaada mkubwa kwa Barcelona na kupelekea kutokupoteza mchezo katika
ligi kuu ya soka nchini Hispania ‘La Liga’ ndani ya michezo saba wakiwa na
kocha mpya Vilanova, ambaye anafuata nyayo za Guardiola na kupelekea klabu hiyo
kupata matokeo mazuri.
Ameendelea kunukuliwa
Xavi akisema
"Pep na
Tito, wanatofauti ndogo sana ya kiufundi, ni kama wana fanana. Guardiola alikuwa
anapenda vitendo, na Vilanova hayuko mbali "
"Tito amekuwa akinishangaza, kwasababu
anaonekana kujiandaa sana, akiwa na mawazo yaliyo wazi na anaendeleza ‘philosophy’
ya klabu.
Robinho amtetea bosi wake Allegri
Mshambuliaji
wa AC Milan Robinho amemtetea kocha wake ambaye yuko katika hali tete juu ya
kibarua chake Massimiliano Allegri, akisisitiza kuwa wachezaji wako nyuma yake.
Rossoneri imeshinda
michezo mitatu katika michezo mbalimbali ya kimashindano mpaka sasa msimu huu
huku hatma ya Allegr ikiingia mashakani tangu kichapo cha bao 1-0 toka kwa
wapinzani wao wakubwa Inter Milan katika ile inayotambulika kama ‘Derby della
Madonnina’ wiki iliyopita.
Akinukuliwa na
Gazzetta dello Sport Robinho amesema,
"Ni
ngumu na msimu hauwezi kuwa umeanza mpaka timu ishinde, Kama Allegri yuko
katika matatizo hata sisi ni hivyo. Lakini mpira wa miguu unatufundisha kuwa
mambo yanaweza badilika haraka"
"inachukua
michezo miwili mpaka mitatu unacheza vizuri lakini baadaye unarudi kule kule.
Mchezo
na Inter, walistahili kushinda lakini hii aibu baada ya kichapo tu, presha imepanda
zaidi.
"haya
mambo ni ya kawaida. Najisikia vibaya kumuona Allegri anaingia katika kipindi
kigumu kama hivi na minong’ono mingi dhidi yake.
Lucas bado anajipa moyo na mataji Liverpool
Lucas Leiva anaamini
kuwa Liverpool inaweza kubadilika na kutoa changamoto mpya katika kutwaa mataji
ya ligi kuu ya nchini England ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo hususani
baada ya klabu hiyo kumuajiri Brendan Rodgers na wachezaji muhimu kuongeza
mikataba.
Wekundu hao
wameshindwa kufuzu klabu bingwa ulaya kwa kipindi cha miaka mitatu sasa, baada
ya matokeo mabovu ya michezo ya ligi , lakini meneja mpya aliye ajiriwa katika
kipindi cha majira ya kiangazi akitokea Swansea Rodgers ameanza kujenga upya
kikosi cha klabu hiyo.
Kitendo cha
kusaini upya mikataba yao kwa wachezaji kama Luis Suarez, Daniel Agger na Martin
Skrtel kunampa imani Lucas mwenye umri wa miaka 25 kuamini Liverpool ina
kikosi ambacho kinaweza kubadilisha hali ya mambo ndani ya kipindi cha miaka
mitano.
Amenukuliwa akisema,
"ndani
ya kipindi cha miaka mitano, nina imani kuwa tunaweza kushinda taji la ligi na
klabu bingwa ulaya. Kwanini isiwezekane? Tunapaswa kuamini hivyo. Hii klabu
inaonyesha wazi kuwa tunaweza kwanini tusirejee katika enzi zile ?"
No comments:
Post a Comment