Bosi wa Anzhi
Makhachkala Guus Hiddink ana matumaini
kuwa inaweza kurejea katika ubora wake kama moja ya timu za kutisha katika ligi
kuu ya soka nchini England.
Bosi huyo wa
zamani wa Uholanzi anatarajia kuwepo uwanjani usiku huu akishusha kikosi chake
katika dimba la Anfield katika mchezo moja ya michezo ya michuano hya UEFA
Europa League dhidi ya wekundu hao baada ya kuanza vema katika michezo yake
miwili ya michuano hiyo na kujikusanyia jumla ya alama nne.
Hiddink alirejesha
nyuma kumbukumbu zake wakati akiwa kocha wa Chelsea kuelekea mwishoni mwa msimu
wa 2008-09, mbapo Liverpool ilikuwa ikitoa upinzani katika kusaka taji la ligi
ya England lakini ikamaliza msimu ikiwa katika nafasi ya pili nyuma ya Manchester
United.
Kocha huyo
mwenye umri wa miaka 65 anaamini kuwa licha ya kuanza vibaya msimu huu kwa wekundu
hao chini ya kocha Brendan Rodgers, lakini wanaweza kurejea katika kiwango safi na
kurejesha enzi zile za utawala wao katika ligi soka la ulaya.
"bila
shaka mwaka 2009 walikuwa na wachezaji
wapya lakini walikuwa wakiongoza ligi"
"msimu huu wamekuwa na matatizo ya kuanza
msimu lakini hii ni taasisi kubwa siku zote inaweza kujirekebisha.
No comments:
Post a Comment