Champions League ni muhimu kuliko ligi
:Arsene Wenger
Arsene
Wenger amesema michezo ya kuwania kufuzu vilabu bingwa Ulaya ni muhimu zaidi ya
kushinda mataji ya FA na League Cup.
Washika mitutu
hao ambao hawajawahi kushinda taji lolote tangu mwaka 2005, kwasasa wako ndani
ya kinyang’anyiro hicho kwa miaka 15 mfululizo.
Akikaririwa meneja
Wenger anasema
"kuna
mataji matano kushindania, la kwanza ni ligi, la pili vilabu bingwsa , la tatu
ni kampeni ya kufuzu vilabu bingwa, nne ni na tano ni kushinda taji la
ligi"
Akaongeza kwa
kusema
"nasema
hivi kwasababu kama unataka kuwapendeza wachezaji bora, hawatakuuliza kama
umeshinda taji la ligi, wanauliza kama unacheza vilabu bingwa ulaya."
Wenger alikuwa
wa mwisho kuongea katika kikao cha wanahisa ambacho kimsingi kilimpongeza.
Hata hivyo
aliomba radhi kwa matokeo ya jana ya ligi ya mabingwa ulaya baada ya kupokea
kichapo kutoka kwa Schalke ambacho kilifuatia kichapo cha ligi kuu toka kwa
Norwich.
"samahani
kwa usiku wa jana "
"najua
haikuwafurahisha mashabiki"
Hotuba ya Wenger
kwa namna moja ama nyingine ilikuwa ni kutuliza hali ya mambo ilivyo juu ya matokeo ya timu yake.
Barcelona wakata rufaa juu ya kifungo
cha Mascherano.
Barcelona imetangaza
kupitia mtandao wa klabu yao kuwa imekata rufaa katika kamati ya rufaa ya ligi
kuu ya nchini Hispania La Liga baada ya Javier Mascherano kupewa kibano cha kusimama
mchezo mmoja kutokana na kuonyeshwa kadi nyekundu wiki iliyopita.
Muarjentina
huyo alikutana na adhabu hiyo katika mchezo ambao Barca walichomza na ushindi
wa mabao 5-4 dhidi ya Deportivo La
Coruna jumamosi baada ya kutanguliziwa kupewa kadi mbili za njano na mwamuzi Jose
Paradas.
Barca
imewasilisha rufaa hiyo dhidi ya taarifa ya mwamuzi iliyowasilishwa baada ya
mchezo, na sasa baaada ya kupitia taarifa iliyoelezea adhabu hiyo wakawasilisha rufaa nyingine dhidi ya kamati hiyo ya rufaa.
Catalans wanaimani
ya kwamba watakuwa na Mascherano katika mchezo wao ujao wa ligi dhidi ya Rayo
Vallecano, akiwa kama mlinzi wa kati wakati huu ambapo Carles Puyol na Gerard
Pique wakiwa bado hawaja rejea kikosini kutokana na kukabiliwa na majeraha.
Mascherano, mwenye
umri wa miaka 28, tangu kuanza kwa msimu huu, ameitumikia timu yake michezo 12.
No comments:
Post a Comment