KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, October 4, 2012

MWALUSAKO AZUNGUMZIA HALI YA YONDANI, KUIKOSA MICHEZO YA KANDA ZIWA.

Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam imeendelea kupata kigugumizi kuzungumzia juu ya hali ya mlinzi wao mahiri Kelvin Yondani ambaye hapo jana alijeruhiwa vibaya na kiungo wa Simba Haruna Moshi maarufu kama Boban katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara, uliokuwa mgumu na kutoa matokeo ya sare ya bao 1-1.
Boban akitokea benchi katika hali isiyotarajiwa alimkita mlinzi huyo katika sehemu ya nyuma ya mguu wa Yandani na kumsababishia maumivu makali ambayo yalipeleka mlinzi huyo kushindwa kuendelea na mchezo kabla ya kuelekea katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kufanyiwa uangalizi wa kina juu ya maumivu hayo.

Akiongea na Rockerspots kaimu katibu mkuu wa Yanga Laurence Mwalusako amesema hali ya mlinzi huyo inaendelea vizuri licha ya maumivu kiasi kuendelea kumsumbua mlinzi huyo hodari.

Mwalusako amesema bado daktari wa timu Dr Sufiani kwa kushirikiana na daktari bingwa wa mambo ya misuli toka Muhimbili wanaendelea kushughulikia hali ya Yondani wakifanya matibabu ya kupunguza maumivu kwa kutumia mionzi (physiotherapy) lakini hata hivyo katibu huyo ameshindwa kueleza kama mchezaji anaweza kurejea kikosini katika siku za hivi karibuni na kuendelea kutoa huduma kama kawaida.

 Taarifa zaidi zinasema huenda Yondani akarejea kikosini baada ya wiki moja na nusu mpaka wiki mbili, hali ambayo itamkosesha miwili ya kanda ya ziwa ambapo Yanga ataanzia mkoani Kagera dhidi ya Kagera Sugar Oktoba 7 na baadaye Oktoba 10 dhidi ya Toto Afrika ya Mwanza kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam Oktoba 17 kucheza dhidi ya Ruvu Shooting.   

Yanga inatarajiwa kuondoka jijini Dar es Salaam jumamosi kuelekea mkoani Kagera kwa ajili ya mchezo wao na Kagera Sugar.
 

No comments:

Post a Comment