KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, November 27, 2012

UGANDA CRANES YAKATA TIKETI YA KWANZA YA ROBO FAINALI YA MICHUANO YA CHALENJI. HARAMBEE STARS NAYO YAIFUNGISHA VIRAGO SUDANI KUSINI.


Brian Umony wa Uganda Cranes mwenye jezi ya njano akifunga goli kwa kichwa katika mchezo dhidi ya Ethiopia.

Uganda Cranes imekuwa timu ya kwanza kufuzu hatu ya robo fainali ya michuano ya chalenji ya Tusker kwa nchi za Afrika Mashariki na kati baada ya kuichapa timu ngumu ya 1-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Mandela ukifahamika zaidi kama uwanja wa Namboole.

Brian Umony ndiye aliyekuwa mfungaji wa bao hilo pekee kunako dakika ya 9 ya mchezo.

Mshambuliaji huyo alifunga goli hilo baada ya kupokea pasi murua ya mshambuliaji anayeshezea klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam Emmanuel Okwi ambaye hapo kabla alikuwa akipokezana pasi na Moses Oloya.

Hilo ni bao la kwanza kwa Brian Umony tangu kuanza kuitumikia timu ya Taifa ya Uganda The Cranes ambapo alifunga goli katika mchezo dhidi ya Malawi March 2009 katika mchezo wa kirafiki katika dimba la Namboole. 

Katika mchezo wa mapema Harambe Stars ya Kenya imefanikiwa kuwafungasha virago timu ngeni katika michuano hiyo ya Sudani Kusini  kwa mabao 2-0
David Ochieng ndiye aliyekuwa wa kwanza kukifungia kikosi cha kocha James Nandwa bao kunako dakika ya 14 ya mchezo akiunganisha mpira wa kona wa Paul Were.

Mara baada ya bao hilo Kenya waliendelea kuutawala mchezo na pengine wangeandika bao la pili kupitia kwa Paul Were ambaye hii leo alinza badala ya Clifton Miheso almbaye alivurunda katika mchezo wa kwanza dhidi ya Uganda.

Kunako dakika ya 76 mchezaji aliyetokea benchi Clifton Miheso alinadika bao la pili kwa Kenya kwa mpira rahisi wa krosi kutoka upande wa kulia na kufanya matokeo kusomeka 2-0.

No comments:

Post a Comment