MENEJA wa Manchester
United Sir Alex Ferguson amekiri kuwa ujio wa Robin van Persie umeimarisha
uwezo wa kikosi chake hususani katika eneo la ushambuliaji.
Akiwa tayari
ameshatupia wavuni jumla ya mabao 15 , mshambuliaji huyo raia wa uholanzi
hajafanya makosa ya kusubiri kujenga jina Old Trafford, huku meneja wake Ferguron mbali ya kumpongeza yeye, lakini pia amekiri
kuwa kwa ujumla kikosi kizima cha United kimebadilika kiuwezo kiasi kupelekea
washambuliaji wote kuonyesha makali yao.
Amenukuliwa Sir
Alex akisema,
“Eneo la
ushambuliaji kwa hakika limeimarika tangu kujiunga kwa Van Persie na kwakweli
ametia nguvu akifunga magoli 14 kabla ya
ushindi wetu wa mabao 3-1 dhidi ya Sunderland mpaka sasa"
"Chicharito
sasa ana magoli tisa, Rooney magoli saba, nadhani nafikiri tuna magoli 43 kama
timu jambo ambalo ni idadi ya juu katika kipindi hiki cha mwaka"
Sir Alex akazidi
kwenda mbele zaidi kwa kutoa maoni yake akilinganisha kipindi hiki cha
ujio wa Van Persie na mwaka 1992 wakati wa ujio wa Eric Cantona, akisema kila mchezaji anahitaji mazingira ya aina yake kuzoea mazingira
"Van
anafanana kisifa na Eric kwa nyakati za ujio unapo zungumzia umri na ukomavu"
"alikuwa
na kipindi kizuri sana wakati wa utumishi wake Arsenal hivyo hakuna haja ya kurubiri kuzoeamazingira
ya Premier League.
"ametokea
katika klabu kubwa na amekuja katika klabu kubwa na amejiamarisha kumataifa,
mambo yote haya ni muhimu kwetu"
PSG imethibitisha kumtaka Mourinho na Cristiano Ronaldo.
Sheikh Bin
Abdulrahman Al-Thani ameweka wazi kuwa Paris Saint-Germain inawataka Cristiano
Ronaldo na kocha wake Jose Mourinho kutoka Real Madrid.
Rais wa PSG Nasser
Al-Khelaifi huko nyuma aliwahi kukaririwa akikanusha taarifa kuwa kigogo hicho cha ligi kuu ya
nchini Ufaransa Ligue 1 kuwa kilikuwa na mpango wa kumsainisha kocha wa Madrid
na Ronaldo lakini mtu wake wa upande wa pili ameibuka na kusema wazi kuwa ili lengo la kutwaa ligi
ya vilabu bingwa Ulaya litimie basi lazima watafute watu muafaka.
Akiongea na
Canal Football amesema,
"Cristiano
Ronaldo na Jose Mourinho ni miongoni mwa malengo yetu hapa Paris Saint-Germain".
"PSG ni
miongoni mwa klabu kubwa duniani. Na hivyo moja ya malengo yetu ni kushinda taji la
vilabu Ulaya.
"ni
klabu kubwa Ufaransa, hivyo lengo ni kuwa klabu bora Ulaya na duniani kwa ujumla"
No comments:
Post a Comment