KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, December 5, 2012

UMESHAWAHI KUMUONA KOCHA JAMHURI KIHWELU WA SERENGETI BOYS ANALILIA NCHI YAKE, BASI HUYU HAPA. TFF YAKUSANYA USHAHIDI WA KUWASHITAKI CONGO BRAZZAVILLE.

Ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo.Kocha msaidizi wa Serengeti Boys Jamhuri Kihwelu akilia mbele ya waandishi wa habari wakati akielezea tukio la kupigwa na askari wa Congo Brazzaville.Bofya hapo chini.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewasilisha barua ya malalamiko yake dhidi ya matumizi ya wachezaji wenye umri
mkubwa na unyanyasaji uliofanyuwa kwa maofisa wa timu ya taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 17 wa Serengeti Boys wakati
wa mechi ya marudiano ya michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Vijana dhidi ya Congo. 

Serengteti Boys iliondolewa kwenye mashindano hayo kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi ya
kwanza iliyofanyika Novemba 18, 2012 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es salaam na baadaye kukubali kipigo cha mabao 2-0 kwenye
mechi ya marudiano jijini Brazaville Jumapili iliyopita. 

Hata hivyo, mechi hizo mbili zilizingirwa na matukio ya utata, hasa kuhusu umri wa wachezaji wa Congo ambao kimaumbile walionekana
kuwa ni umri mkubwa zaidi na kusababisha TFF kuwasiliana na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika (CAF) kuhusu njia zinazowezekana
kupata uthibitisho wa umri wa wachezaji hao, lakini ilishindikana na ndipo TFF ilipocheza mechi hiyo ikiwa na imeweka pingamnizi.
Katika barua iliyotumwa CAF jana, TFF imerejea barua ya pingamizi aliyokabidhiwa kamisaa wa mechi ya kwanza jijini Dar Es salaam,
Bw. Chayu Kabalamula na malalamiko yaliyowasilishwa kwa kamisaa wa mechi ya marudiano kuhusu vurugu walizofanyiwa maofisa wa
timu.
Katika barua hiyo, TFF imeomba CAF iagize kuwa wachezaji wote wa Congo waliocheza mechi hizo mbili wapimwe tena kwa kutumia
kipimo cha M.R.I na gharama za zoezi hilo zilipiwe na TFF; na pili Shirikisho limeomba kuwa CAF ikubali kuipa Tanzania wiki tatu za
kukusanya ushahidi na kuuwasilisha Cairo kwa ajili ya maamuzi.
Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo, nchi shiriki zinatakiwa kuwapima wachezaji wake kwa kutumia kipimo cha M.R.I ambacho
kinaweza kutambua umri wa vijana walio chini ya miaka 17 na kwamba matokeo yake yanatumwa CAF, ambayo itahifadhi matokeo hayo
hadi hapo kutakapotokea pingamizi na ndipo itafanyia kazi kwsa kutoa matokeo ya vipimo hivyo.
“Ni matumaini yetu kuwa suala letu litafanyiwa kazi na kutolwewa ufumbuzi ili kulinda soka la vijana barani Afrika dhidi ya vitendo
vilivyokomaa vya udanganyifu wa umri,” alisema katibu mkuu wa TFF, Angetile Osiah.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari hii leo, kocha Jacob Michelsen amesema alishangaa kuona wachezaji wenye umri
mkubwa zaidi wakichezeshwa kwenye mechi ya marudiano, lakini akaisifu TFF kuwa inafuata njia sahihi ya maendeleo na haina budi
kuendelea na programu yake ya soka la vijana.
"Najivunia vijana wangu kwa kuwa walijituma kwa muda wote pamoja na kwamba wenyeji waliongeza wachezaji wenye umri mkubwa
zaidi kuliko waliokuja huku," alisema kocha huyo kutoka Denmark.
"Kitu cha msingi ni kufuata njia sahihi ya kuendeleza soka na natumaini TFF iko kwenye njia sahihi na itaendelea na programu yake ya
vijana. Hakuna njia ya mkato kama mnataka maendeleo. Ni lazima tufuate njia sahihi na matunda yake tutayaona baadaye.
"Kila mara nasema mambo (ya vijana) huchukua muda mrefu (Things Take Time) na hivyo hatuna budi kuwa wavumilivu.
"Wenzetu walitumia njia za ajabu na hata hiyo penati ya bao la kwanza haikuwa faulo. Ilitokea nje kabisa ya eneo la penati. Refa
alimuangalia kibendera akaona ametulia, akamuangalia beki mchezaji akamuona amesimama, mara akaangalia juu na kupuliza filimbi
kuonyesha kuwa ni penati."
Naye kocha msaidizi, Jamhuri Kihwelo alishindwa kujizuia na kujikuta akibubujika machozi wakati alipoelezea jinsi alivyoshambuliwa na
askari kabla ya mchezo huo.

No comments:

Post a Comment