Olympiakos iliyotokea
nyuma imefanikiwa kuichapa Arsenal mjini Piraeus, na kuwafanya washika mitutu
hao kumaliza katika nafasi ya pili katika kundi B nyuma ya Schalke.
Tomas Rosicky
alianza kufunga bao la uongozi kwa Arsenal kabla ya bao la kipindi cha pili la Giannis
Maniatis lililokuwa la kusawazisha na baadaye Kostas Mitroglou kuandika bao la
pili na la ushindi kwa wagiriki.
Kocha wa
Schalke Leonardo Jardim aliwatumia wachezaji wake ambao ni wafungaji wakubwa
katika ligi ya Ugiriki Rafik Djebbour na
Djamel Abdoun sehemu ya kiungo.
Akiwa ni
mwenye matumaini ya kufuzu, Wenger alikifanyia mabadiliko kikosi chake
kilichopoteza dhidi ya Swansea mabao 2-0 mwishoni mwa juma akimrejesha Rosicky kiungoni
pamoja na kinda wa miaka 20 Jernande Meade akicheza dakika zote za mchezo.
MANCHESTER CITY 0 VS DOTMUND 1
Manchester
City imemaliza kampeni ya michuano ya ligi ya mabingwa ulaya kwa kichapo
kingine cha bao 1-0 toka Borussia
Dortmund.
Bao la
kipindi cha pili la Julian Schieber kunako dakika ya 57 lilitosha kuwaondosha katika
harakati za kusonga mbele na michuano hiyo huku wajerumani wakifurahia mchezo
ambapo walitengeneza nafasi nyingi karibu sehemu kubwa ya mchezo.
Matokeo hayo
yana maanisha kuwa kikosi cha Roberto Mancini kimemaliza michezo yake ya kundi
D kikiwa mkiani bila ushindi hata mmoja na Dortmund wakifanikiwa kusonga mbele
katika hatua ya mtoano ya michuano hiyo.
- MATOKEO MENGINE
- Din Zagreb 1 - 1 Dynamo Kiev FT
- Malaga 2 - 2 Anderlecht FT
- Montpellier 1 - 1 Schalke 04 FT
- Paris SG 2 - 1 FC Porto FT
- Real Madrid 4 - 1 Ajax FT
No comments:
Post a Comment