Timu ya
taifa ya Uganda ‘Uganda Cranes’ imepiga hatua nyingine muhimu ya kucheza hatua
ya nusu fainali ya michuano ya Cecafa Tusker Cup 2012 baada ya kuichapa timu
ngumu ya Ethiopia mabao 2-0 mchezo wa robo fainali uliochezwa katika
dimba la Mandela lililopo katika kitongoji cha Namboole jioni ya leo.
Geoffrey
‘Baba’ Kizito na Robert Ssentongo ndio waliokuwa wafungaji wa mabao hayo.
The Cranes sasa
itakutana na Kilimanjaro Stars ambayo ilitinga nusu fainali baada ya kuichapa
timu ya taifa ya Rwanda Amavubi kwa mabao nusu fainali itakayopigwa jioni ya
alhamisi.
KATIKA MCHEZO MWINGINE WA MAPEMA
Kenya imeungana
na timu za taifa za Zanzibar na Kilimanjaro Stars kucheza hatua ya nusu fainali
ya michuano ya Cecafa Tusker Cup 2012 baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa bao
1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Malawi ambao walikuwa ni waalikwa katika michuano
ya mwaka huu mchezo uliopigwa katika dimba la Mandela lililoko katika kitongoji
cha Namboole.
Mike Barasa ndiye
aliyefunga bao pekee la washindi ambalo limeifanikisha Harambe Stars kutinga
nusu fainali ua michuano hiyo ya 34 ambayo ni mikongwe kuliko yote barani
Afrika.
Harambe Stars sasa itakutana na mabingwa wa
mwaka 1995 Zanzibar ambao wamewaondosha Burundi
mabao 6-5 kwa njia ya penati katika hatua ya robo fainali
No comments:
Post a Comment