KLABU ya Yanga leo imezindua kalenda yake ya mwaka 2013 katika hafla
iliyofanyika makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Jangwani, Dar es Salaam.
Uzinduzi wa kalenda hiyo ulifanywa na Katibu Mkuu wa klabu hiyo,
Lawrence Mwalusako.
Mbali na uzinduzi wa kalenda, Yanga pia ilizindua klabu ya mashabiki wake, ambao ili kujiunga watalazimika kutuma ujumbe wa simu wa maandishi sms.
Hafla hiyo ilipambwa na wacheza shoo wa kikundi kimoja cha burudani cha mjini Dar es Salaam. Yanga imepanga kuziuza kalenda hizo kwa mashabiki wake nchi nzima kwa lengo la kujiongezea mapato.
(Habari, picha na Emmanuel Ndege wa liwazozito)
No comments:
Post a Comment