Christopher Samba ameelekea jijini London kukamilisha taratibu za mwisho za kujiunga na QPR baada ya timu hiyo isiyo na matokeo mazuri katika ligi kuu ya nchini England kukubali sharti la kutakiwa kutoa pauni milioni £12.5 kufanikisha kumtoa katika mkataba wake wa sasa.
Samba anataka kuondoka Anzhi Makhachkala ambapo meneja wake Guus Hiddink amekuwa akipingana na mpango wa kuondoka kwa mchezaji huyo.
Hiddink amekaririwa akisema,
'Samba ameelekea England jana. Nadhani kati ya leo au kesho itafahamika nini kitatokea.
'Ni aibu kulizungumzia hili lakini hakutuaga, hakutuambia lolote kuhusu hilo.
'Unajua kwa lolote unalotaka kufanya unapaswa kuwashirikisha watu unaofanya nao kazi.
'Hakuna tatizo. Tulianza naye maandalizi ya msimu lakini ghafla akaanza mawasiliano na England akiwa bado ana mkataba na Anzhi.'
No comments:
Post a Comment