KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, January 29, 2013

TANZANIA PRISONS KUMKOSA EMMANUEL GABRIEL MWAKYUSA MPAKA WAKAMILISHE TARATIBU ZA ITC.

Emmanuel Gabriel Mwakyusa.
 Klabu ya Tanzania Prisons itaendelea kumkosa mshambuliaji Emmanuel Gabriel 'Mwakyusa' mpaka hapo watakapo kamilisha taratibu za uhamisho wa kimataifa ITC kutoka klabu ya Rayol Sports ya Rwanda.
Gabriel alilazimika kuondolewa katika orodha ya wachezaji wa kikosi cha kwanza kilichokuwa kikicheza dhidi ya Yanga jumapili uwanja wa taifa ukiwa ni mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara ambapo Prisons ililala kwa mabao 3-1.

Akilitolea ufafanuzi sakata la Gabriel afisa habari wa shirikisho la soka nchini TFF Bonface wambura amesema kwa kumbukumbu za TFF ni kwamba mchezaji huyo alikuwa kicheza soka nje ya nchi hususani nchini Rwanda na TFF ndiyo waliotoa hati ya uhamisho wake wa kimataifa ITC kuelekea nchini humo hivyo Prisons watalazimika kuisaka ITC ya kumrudisha mshambuliaji huyo nchini kama taratibu zinavyotaka.

Gabriel mshambuliaji wa zamani wa mabingwa wa soka Tanzania bara Simba, aliombewa uhamisho wa kujiunga na Tanzania Prisons kwa ajili yaa duru la pili la ligi kuu ya soka Tanzania Bara na jumapili alikuwemo katika orodha ya wachezaji wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo lakini alizuiliwa kuingiwa uwanjani kutoka na kasoro zilizoonekana mapema kabla ya kuanza kwa mchezo huo.

Lakini wakati hayo yakiwa hivyo taarifa zinasema kuwa tayari Emmanuel Gabrie alisharejea nchini siku nyingi na kwamba alikuwemo katika kikosi cha timu ya AFC katika msimu wa 2010/2011 na alitumiwa na timu hiyo katika ligi soka daraja la kwanza na kufanikisha kuipandisha daraja timu hiyo huku TFF wakiwa hawana habari.
Bofya chini kusikiliza

No comments:

Post a Comment