KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, May 13, 2013

Aubameyang ashinda tuzo ya marehemu Marc-Vivien.



Mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang ametajwa kuwa mshindi wa tuzo ya mwaka 2013 ya Marc-Vivien Foe Prize tuzo ambayo ilitolewa jumatano nchini Ufaransa baada ya kumshinda mcameroon Nicolas Nkoulou na mwingine kutoka Burkina Faso Jonathan Pitroipa. 

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 akikipiga na Saint Etienne amefunga jumla ya magoli 209 na kuwashinda mshambuliaji wa  Marseille Nkoulou, aliyepeta kura 81 mchezaji bora wa michuano ya mataifa ya Afrika Jonathan Pitroipa akipata alama 35.

Jumla ya waandishi wa habari za michezo 68 walishiriki katika kupiga kura hiyo ambayo imempa ushindi mfungaji huyo wa  pili katika ligi kuu ya soka ya nchini Ufaransa Ligue 1 kuwa mrithi wa Younes Belhanda wa Morocco ambaye alishinda tuzo hiyo mwaka jana. 

Tuzo ya Marc-Vivien Foe ilianzishwa mwaka 2009 kwa lengo la kumska mchezaji bora wa msimu wa kiafrika wanaochezea ligi kuu ya nchini Ufaransa French Ligue 1 ikiwa ni kumuenzi nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Cameroon ambaye alizimia na kufia uwanjani mwaka 2003 wakati wa michuano ya Fifa ya Confederations mchezo wa nusu fainali baina ya Indomitable Lions dhidi ya Colombia mjini Lyon, Ufaranza.

No comments:

Post a Comment