Carlo Ancelotti |
Rais wa Paris Saint-Germain amedai kuwasiliana na Real Madrid juu ya kusudio lao la kumtaka meneja wao Carlo Ancelotti kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.
Taarifa hizo zimezidi kutia utambi habari za kigogo hicho cha Hisapani kuachana na Jose Mourinho majira ya kiangazi.
Meneja huyo Mreno amekuwa akihusishwa sana na kurejea Chelsea.
Mwenyekiti wa PSG Nasser Al-Khelaifi ameliambia gazeti la L'Equipe kuwa
'siku
kadhaa zilizopita meneja mkuu wa Real Madrid Jose Angel Sanchez
amewasiliana na mimi kuzungumzia kuwa nizungumze na Ancelotti.
'Haraha
sana nikamwambia kama mnataka Carlo, unapaswa kujua kuwa bado ana
mkataba wa mwaka mmoja hivyo basi tafadhali heshimu mkataba wetu.
'Tunaziheshimu
klabu zote, tunategemea kuwa na majibi kama hayo. Leo hatuna hadhi kama
ya Real Madrid, lakini tunastahili heshima'.
'Aliniomba
radhi na kuniambia alidhani mkataba wa Ancelotti's ulikuwa umemalizika
lakini nilimwambia kuwa alikuwa amekosea na kwamna Carlo bado ana mwaka
mwingine mmoja, na kusema wanaheshimu hilo'
Ancelotti
aliingia PSG December 2011, na kumaliza katika nafasi ya pili lakini akafanikiwa kutwaa taji msimu huu.
Hapo kabla alikuwa ni meneja wa Chelsea kabla ya kufukuzwa kwa karaha na mmiliki wake Roman AbramovichMay 2011.
Carlo Ancelotti anayekumbatiana na David Bekham.
Mourinho.
Zlatan Ibrahimovic anasema anataka kusalia katika jiji la na anataka Ancelotti kusalia kazini ambapo msweden huyo amekaririwa akisema.
'Amefanya kazi kubwa msimu huu,'
No comments:
Post a Comment