CESC FABREGAS KUSAJILIWA NA MANCHESTER UNITED.
|
Klabu ya Manchester United imewasilisha ombi la kutaka kumsajili mcheza kiungo wa klabu ya Barcelona Cesc Fabregas.
Ripoti zinasema kuwa Manchester United inataka
kumsajili mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal kwa kitita cha pauni
milioni ishirini na tano.
Wasimamizi wa Barcelona kwa sasa wanajadili pendekezo hilo, lakini inaaminika kuwa kiasi walichopendekeza ni kidogo.
Licha ya kuwa Fabregas hajaomba kuruhusiwa kuondoka, lakini kuna fununu kuwa huenda akashawishika kurejea tena nchini England.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, huenda
akakubali kujiunga na Manchester United ikiwa wasimizi wa Barcelona
watakubali kiasi kilichopendekezwa na Manchester United.
|
|
Wanariadha wawili kati ya wanariadha wenye kasi kubwa
duniani Tyson Gay, kutoka Marekani na Asafa Powell wa Jamaica
wamepatikana na kosa kutumia madawa ya kusisimua misuli.
Gay, ambaye ni mwanariadha wa pili kwa kuwa na
kasi kubwa ya kukimbia katika mbio za mita mia moja, amesema anajiondoa
kwenye mashindano ya dunia ya riadha yanayotarajiwa kufanyika mjini
Moscow mwezi ujao.
Asafa Powell, ambaye alishikilia rekodi ya mbio
za mita 100 hadi ilipovunjwa na Usain Bolt mwaka 2008, amekanusha kuwa
alitumia dawa hizo makusudi.
Mwanariadha mwenzake wa Jamaica Sherone Simpson pia amepatikana na hatia ya kuzitumia dawa hizo za kusisimua misuli. |
No comments:
Post a Comment