Zimbabwe imefanikiwa
kutinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Cosafa baada ya kufanikiwa
kuwachapa Malawi kwa mikwaju ya penati baada ya kwenda sare ya bao 1-1 katika
muda wa kawaida wa mchezo wao wa hatua ya robo fainali katika mchezo
uliofanyika hii leo huko Kitwe nchini Zambia.
Ocean
Mushure alifunga penato ya ushindi kwa washindi hao mara nne wa michuano hiyo.
Katika muda
wa kawaida Zimbabwe walikuwa wa kwanza
kushambulia na kuandika bao la uongozi kwa mpira wa kurudi uliofungwa na Masimba
Mambare kunako dakika ya.
Mshambuliaji
wa Malawi James Sangala alitolewa nje yaw a uwanja baada ya kupewa kadi ya pili
ya njano kabla ya mapumziko kitendap
ambacho kiliivuruga the Flames.
Lakini hata
hivyo kunako dakika ya 85 ya mchezo , Boniface Kaulesi alifanikiwa kuandika bao
la kuswazisha na mchezo kuelekea katika dakika za nyongeza na hatimaye kufikia
katika hatua ya mikwaju ya penati.
Katika hatua
nyingine Afrika ya kusini nao wamefanikiwa kutinga katika hatua hiyo ya nusu
fainali baada ya kuwachapa Namibia kwa bao 2-1 mchezo ambao pia umepigwa hii
leo.
Bafana
Bafana walikuwa wakicheza mechi yao kwanza ya michuano hiyo kufuatia kupata
nafasi ya kuingia moja kwa moja katika hayua hiyo
Mchezaji alieingia
kutoka benchi Shongwe Jabulani aliandika bao kwanza kwa mpira mrefu muda mfupi
baada ya kuanza kipindi cha pili.
Afrika
kusini pia wakafanikiwa kuandika bao la pili kupitia kwa Kekana Hlompho akiwa
katika kona ya kisanduku cha hatari.
Namibia walifanikiwa
kupata penati kufuatia Mkhwanazi Buhlke kuunawa mpira ndani ya kisanduku cha 18
lakini hata hivyo
Willy
Stephanus alishindwa kuandika bao kwa pigo la kwanza kabla ya mwamuzi kumtaka
kurudia penati yake ambapo kiungo huyo aliiukwamisha mpira kambani.
No comments:
Post a Comment