Rooney haendi kokote asema Moyes
Kocha mpya
wa Manchester United David Moyes, amekariri kuwa nyota wake Wayne Rooney
atasalia na klabu hiyo na kamwe hana nia yoyote ya kumuuza mchezaji huyo.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 27, anarejea nyumbani kutoka Thailand ambako timu
hiyo imepiga kambi kambla ya kuanza kwa msimu, kutokana na jeraha la mguu.
Kumekuwa na
fununu kuwa mchezaji huyo huenda akakihama klabu hiyo, licha ya Moyes
kusisitiza kuwa Rooney hauzwi kwa lolote lile.
Klabu ya
Chelsea, vile vile wako nchini Thailand na kocha wao mpya Jose Mourinho
aliulizwa ikiwa ana nia ya kumsajili Rooney.
Lakini
Mourinho alisema kwamba hana mazoea ya kuzungumza kuhusu wachezaji wa klabu
nyingine lakini amekiri kuwa anampenda Rooney.
Kwa upande
wake Moyes alisema kocha huyo wa Chelsea ana nia ya kumsajili mchezaji huyo ila
hataki kusema wazi wazi.
Rooney,
ambaye ameifunguia Manchester United magoli 197, baada ya kucheza mechi mia nne
na mbili anatarajiwa kusalia nje ya uwanja wa muda wa wiki mbili zijazo
kutokana na jeraha hilo na wala sio mwezi mmoja kama ilivyokuwa imetangazwa
hapo awali.
Mmiliki mpya wa Fulham Shahid Khan anataka
kuipelekea klabu hiyo katika kiwango kingine.
Mmiliki mpya
wa klabu ya Fulham Shahid Khan ana matumaini ya kuijenga klabu hiyo kwa
kufanyia kazi yale mtangulizi wake Mohamed Al Fayed.
Al Fayed
mwenye umri wa miaka 84, aliinunua Fulham mwaka 1997 na kuifanya klabu hiyo
kuwa moja ya klabu bora katika ligi kuu ya soka nchini England tangu mwaka 2001.
Billionaire
Khan ambaye ana umri wa miaka 62 kwasasa ameinunua klabu hiyo kutoka kwa Al
Fayed ambapo amenukuliwa akisema klabu hiyo ni sehemu muafaka na eneo muhimu
kwa wakati muafaka.
Mzaliwa huyo
wa Pakistan alielekea nchini Marekeani wakati akiwa na umri mdogo wa miaka 16 na
kuanza kujishughulisha na biashara ya spea za magari.
Baadae akawa
mmiliki wa timu ya NFL ya Jacksonville
Jaguars mwezi Desemba mwaka 2011 na sasa anakuwa mmiliki wa sita wa klabu kubwa
nchini England inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini humo Premier League.
Fulham
ilifikia katika hatua ya fainali ya michuano ya Europa chini ya meneja Roy
Hodgson mwezi Mei mwaka 2010, ambapo walifungwa katika fainali na Atletico
Madrid.
Msimu uliopita
ilikuwa chini ya meneja Martin Jol ambapo ilimaliza katika nafasi 12
Real Madrid yamsajili Asier
Illarramendi kwa ada ya pauni milioni 34 akitokea Real Sociedad
Real Madrid imemsajili
kiungo wa Real Sociedad Asier Illarramendi baada ya kukubali kulipa euro
milioni 39 sawa na pauni milioni £34
Nyota huyo
mwenye umri wa miaka 23 anayechezea timu ya taifa ya Hispania ya vijana
amesaini mkataba wa miaka sita na kuwa mmoja wa vijana wa the Bernabeu tayari amefanikiwa
kupita katika vipimo vya afya.
Illarramendi
aliyetokea Sociedad, alikuwa msaada mkubwa katika klabu hiyo msimu uliopita
ambapo aliiwezesha kumaliza katika nafasi ya nne na kupata nafasi ya kucheza
ligi ya mabingwa Ulaya.
Pia amechezea
michezo yote ya timu ya taifa ya vijana Hispania katika michuano ya European
Under-21 nchini Israel mapema msimu huu wa kiangazi.
Illarramendi
anakuwa ni mchezaji wan ne kusajiliwa na kocha mpya wa Real Madrid Carlo
Ancelotti baada ya kocha huyo kufanikisha usajili wa Isco aliyetokea Malaga kwa
ada ya pauni milioni £23, Dani Carvajal aliyejiunga na klabu hiyo akitokea Bayer
Leverkusen na Casemiro aliyejiunga na Madrid kwa mkopo akitokea Sao Paulo sasa
akipewa mkataba wa kudumu.
Alessandro
Nesta aponda ligi kuu ya Italia
Mlinzi wa
kati wa zamani wa kimataifa wa Italia Alessandro Nesta amesema ligi kuu ya soka
nchini humo Serie A imeshindwa kufua dafu kwa ubora mbele ya ligi nyingine za
barani Ulaya ikiwemo ligi ya Hispania, Ujerumani na England.
Nesta ambaye
kwasasa ana umri wa miaka 37 kwasasa anachezea soka katika klabu ya Montreal
Impact inayoshiriki ligi kuu ya Marekani MLS.
Akiwa bado
nchini Italia Nesta aliwahi kushinda taji la Italia maarufu kama Scudetto mara
tatu akiwa na vilabu vya Lazio na AC Milan.
Nesta ametoa
sababu ya kushindwa kwa ligi hiyo ya Italia na ligi nyingine ni kwamba
kumetokana na kukosekana kwa fedha.
Akinukuliwa
amesema
"Hakuna
pesa kwasasa inchini Italia na hivyo wachezaji wazuri wamekuwa akikimbilia
kucheza soka katika ligi za Hispania , England na Ujerumani. Ligi ina poromoka"
Nesta, ambaye
pia alishinda taji la kombe la dunia mwaka 2006, ameshangazwa na klabu ya Juventus
kufanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Carlos Tevez kwa ada
iliyotajwa kuwa ni pauni milioni £12.
Amesema klabu
hiyo imefanya usajili bora kwa kudaka saini ya Tevez, na kwamba hakuwahi
kufikiria mchezaji kama Tevez kuelekea katika ligi ya Italia Serie A kwasasa. Amesema
Juventus imefanya kazi kubwa.
Nesta anataka
kuelekea katika kazi ya ukocha itakapo fikiwa wakati wake wa kustaafu kucheza
mwishoni mwa msimu ujao wa ligi kuu ya Marekani Major League Soccer .
No comments:
Post a Comment