Hali ya wasiwasi kuhusu na fainali ya kombe la dunia mwaka
2022 na wapi lifanyike, imechukua sura mpya baada ya viongozi wa soka
Ulaya kukubali kuwa fainali hiyo haiwezi kuchezewa nchini Qatar wakati wa
majira ya joto.
Nchi hiyo ilipata nafasi ya kuandaa michuano
hiyo kwa njia ambayo wengi wamepinga ikisemekana viwango vya joto nchini
Qatar vinaweza kufika nyuzi hamsini majira ya joto.
Wanachama 54 wa shirikisho la Uefa waliunga mkono hatua hiyo wakati wa mkutano wao nchini Croatia.
"tulichaofikana katika mkutano huu ni kuwa
michuano ya kombe la dunia haiwezi kuchezewa nchini Qatar wakati wa
majira ya joto" alisema naibu rais wa shirikisho la soka duniani FIFA
nchini Uingereza, Jim Boyce.
"kila mtu alikubaliana na wazo hilo.''
Greg Dyke: aliongeza kuwa "michuano hii haiwezi kuandaliwa wakati wa majira ya joto nchini Qatar.''
Kwa mujibu wa Boyce, mjadala wa sasa ni ikiwa dimba hilo lifanyika Januari 2022 au mwezi Nivemba ama Disemba mwaka huo.
Mashirikisho ya Uingereza yanalinda maslahi yao
yakisema kuwa yanataka kuhakikisha kuwa dimba hilo halihitilifiani na
mechi za ligi ya Uingereza wakati Uefa inapendekeza ifanyike Januari ili
isiweze kuathiri ligi ya mabingwa wa Ulaya .
Hata hivyo wanasisitiza kuwa hawataki FIFA kuharakisha uamuzi huo.
"bado kuna miaka tisa mbele yetu na watu wanhisi
kuwa ni sawa kwa FIFA kukaa na washika dau kujadiliana kuhusu swala
hilo na kuwa na mwafaka ambao hautaathiri ligi nyinginezo,'' alisema
Boyce
No comments:
Post a Comment