Malkia wa Uingereza ameanzisha rasmi mbio za
kupokezana rungu la michezo ya Jumuiya ya Madola itakayofanyika mjini
Glasgow Scotland mwaka 2014.
Rungu hiyo ina risala aliyoiandika kwa mkono
Malkia kwa Jumuiya ya Madola itakayosafirishwa katika mataifa na maeneo
yote 70 yatakayoshiriki katika michezo hiyo katika kipindi cha siku 288
zijazo.
Rungu hilo litasafirishwa kwanza
hadi Scotland mnamo siku ya Alkhamisi kabla ya kuelekea India kwa kituo
chake cha kwanza cha kimataifa Octoba 11.
Safari ya rungu hilo itamalizika wakati wa
sherehe za ufunguzi za michezo hiyo Julai 2014, ambapo Malkia ataisoma
risala iliyomo ndani yake.
Katika sherehe za uzinduzi ziliofanyika katika
kasri ya Malkia mjini London, rais wa Shirikisho la michezo ya
Commonwealth , Prince Imran wa Malaysia, amesema mbio za rungu hilo lina
ujumbe mzito wenye maana.
"mbio za kupokezana rungu hilo zinawaunganisha
raia billioni 2 wa Commonwealth katika kusherehekea michezo,kabila
tofauti na amani na kudumisha urafiki na uhusiano wetu" alisema Imran
Baada ya hotuba Malkia alitumbukiza waraka wenye
risala yake ndani ya rungu hilo na kisha kufungwa kwa safari yake ya
kilometa 190,000 kupitia mabara ya Asia, Oceania, Afrika, Amerika za
Kaskazini na Kusini na Caribbean.
Wa kwanza kukimbiza rungu hilo alikua Alan
Wells,mwanariadha wa mbio fupi wa Scotland aliyeshinda medalli ya
dhahabu katika mbio za mita 100 za Olimpiki ya 1980 mjini Moscow.
No comments:
Post a Comment