Kenya kwa mara nyingine tena watakosa huduma ya mshambuliaji wake Jacob Keli wakati wa mchezo wa fainali ya michuano ya chalenji dhidi ya Sudan mchezo ambao utapigwa uwanja wa Nyayo hapo kesho.
Mshambuliaji huyo wa kati wa KCB FC anasumbuliwa na misuli maumivu ambayo aliyapata wakati wa robo fainali dhidi ya Rwanda ambao Kenya ilishinda kwa bao 1-0 mchezo uliochezwa uwanja wa manispaa ya Mombasa ambapo alishindwa kurudi uwanjani katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Kilimanjaro stars ambapo Kenya pia walishinda kwa bao 1-0.
“sijisikii vema,”
Amenukuliwa Keli akiongea na mtandao wa habari za michezo wa Kawowo Sports.
“nasumbuliwa na msuli na sina hakika kama nitacheza mchezo ujao lakini tutaona hali itakavyokuwa” ameongeza Keli.

Wakati huohuo nahodha wa Kenya Allan Wanga anaamini kuwa kocha wake Adel Amrouche atakuja na mbinu stahiki kuelekea katika mchezo wa fainali dhidi ya Sudan mchezo ambao utachezwa uwanja wa Nyayo kesho.
Sudan imekuwa ikielezewa na watazamaji na wajuzi wa mambo ya soka kuwa kikosi cha Sudani kimekuwa bora kiufundi ndani ya michuano hii lakini Wanga ana matumaini kuwa kocha wa Harambee
Stars atakuwa na mbinu bora zaidi ya Sudan.
Fainali hiyo itakuwa ikipigwa hiyo kesho ambayo ni siku ya uhuru wa Kenya December 12.
Kwa mara ya mwisho Kenya kuchukua taji hilo ilikuwa 2002.
No comments:
Post a Comment