Kiungo wa timu ya taifa ya Kenya Teddy Anthony Akumu anaamini kuwa mchezo wa nusu fainali dhidi ya Tanzania bara Kilimanjaro Stars ndio uliokuwa mgumu kuliko yote waliyocheza mpaka kufikia sasa katika michuano ya GOtv Cecafa Challenge Cup michuano ambayo sasa imefikia fainali.
Wenyeji hao waliwafunga Kilimanjaro kwa bao 1-0 katika mchezo ambao ulikuwa mgumu kwa sehemu kubwa ya mchezo na ambao Kilimanjaro walicheza sehemu kubwa wakitawala.
Hata hivyo mchezo huo uliochezwa uwanja wa Nyayo ulikumbwa na kadhia ya kuchezwa kwenye matope na huku Kenya wakiendelea kushukuru bao lao la mapema lililofungwa na Miheso ambapo Akumu anasema mchezo huo ulifanana na vita uwanjani.
“Ilikuwa ni kama vita dhidi ya Tanzania lakini tunamshukuru Mungu tumefanikiwa kushinda” Akumu amenukuliwa na Kawowo Sports muda mfupi baada ya mchezo huo jana.
“Tanzania walitupa mchezo mgumu lakini kwa bahati tumeshinda na tumetinga fainali” ameongeza.
Kiungo huyo wa Gor Mahia FC alipata tuzo ya mchezaji wa mchezo (Man of the match) baada ya kuonyesha soka zuri sehemu ya kiungo.
Kenya wanawasubiri Falcons wa Sudan katika fainali ya michuano hiyo ambayo itachezwa kesho uwanja wa Nyayo.
No comments:
Post a Comment