KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, December 11, 2013

Juventus hawana mpango na Alksandar Kolarov wa Man City ni uzushi

 Mkurugenzi mtendaji wa kibibi kizee cha Turin Juventus Giuseppe Marotta amekanusha taarifa zilizo anza kuenea kuwa vinara hao wa ligi kuu ya nchini Italia Serie A walikuwa na mpango wa kumsajili mlinzi wa Manchester City Aleksandar Kolarov.
Kolarov mwenye umri wa miaka 28 kwa mara nyingine tena amekuwa akihusishwa na taarifa za kuelekea Bianconeri ikielezwa kuwa alikuwa akiivutia na kuitoa mate Juve.

Hata hivyo Marotta amesisitiza kuwa Juventus hawafikirii kumchukua mlinzi huyo wa kimataifa wa Serbia hata kwa mpango wa kubadilishana mwezi januari.

"Ni wazi kuwa Kolarov ni mwenye thamni, lakini hakuna makubaliano yaliyofanyika hivi sasa hatuna dhamira ya kulianzisha hilo.
Kolarov alijiunga na Manchester City akitokea Lazio miaka mitatu iliyopita na kwasasa yuko ndani ya mkataba wa miaka mitatu mpaka Juni 2015.

No comments:

Post a Comment