Mlinzi wa Bayern Munich Jerome Boateng amekuabli kuongeza mkataba wa miaka mitatu na mabingwa hao wa Ulaya huku akitumia maneno kuwa ni heshima kwake kuendelea kuichezea klabu hiyo.
Mpango huo kwa mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 25 utamuweka ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake Allianz Arena mpaka 2018.
Akinukuliwa na mtandao rasmi wa klabu hiyo amesema
"Bayern ni moja kati ya vilabi vikubwa duniani"
"kucheza hapa si tu kama kazi, bali pia ni heshima.
"nataka kufanikiwa mengi na timu yangu miaka ijayo."
Mkurugenzi mkuu wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge pia ametanabaisha kuwa amefurahishwa na habari za Boateng kwani ni mchezaji muhimu ndani ya kikosi cha kocha Pep Guardiola.
"Ni mmoja wa wachezaji wakubwa ndani ya Bayern".
"kwasababu hiyo ni wazi tumeendelea kuimarisha kikosi kwa kuongeza mkataba wake"
Boateng alijiunga na Bavarians mwezi Julai 2011 baada ya kuitumikia kwa muda mfupi Manchester City na alikuwepo uwanjani jana wakati wakipata kichapo cha mabao 3-2 toka kwa klabu yake ya zamani ya Manchester City.
Ametoa huduma ndani ya klabu hiyo kwa michezo 106 na kuisaidia timu ya taifa ya Ujerumani mara 36 tangu ajiunge nayo mwaka 2009.
No comments:
Post a Comment