Makamu wa Rais wa AC Milan Adriano Galliani amethibitisha kuwa kiungo mshambuliaji wa CSKA Moscow Keisuke Honda atajiunga na klabu yake kwa uhamisho huru Januari 3.
Ntoya huyo wa kimataifa wa Japan hapo kabla alikuwa ajiunge na Milan maarufu kama Rossoneri kabla ya kuanza kampeni za msimu wa 2013-14 lakini klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya soka ya nchini Italia Serie A ilishindwa kukamilisha mipango ya makubaliano na CSKA kuhusina na ada ya uhamisho wake ambapo walitaka uwe huru.

Hata hivyo Galliani ametangaza hii leo kuwa Honda mwenye umri wa miaka 27 atawasili San Siro wakati wa mapumziko ya kipindi cha baridi.
"Honda atakuwa mchezaji wa Milan January 3 na atavalia jezi nambari 10 " Galliani ameeleza hayo kwa waandishi wa habari.
"sijui kama atakuwa tayari kwa ajili ya mchezo wa January 6 dhidi ya Atalanta kutokana na mchakato wa makaratasi ya uhamisho"
Honda aliaanza kucheza professional football akiwa na klabu ya Nagoya Grampus na alikuwa akivalia jezi nambari VVV kabla ya kujiunga na CSKA January 2010.
No comments:
Post a Comment