Mmiliki na mwenyekiti wa timu ya soka ya TP Mazembe
kutoka Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo Moise Katumbi amesema ana mpango
wa kuiimairisha timu hiyo ili iwe na nguvu ya kushiriki katika
mashindano ya kidunia, Katumbi anaamini kuwa anaweza kuifikisha timu
hiyo katika ngazi ya fainali za kombe la dunia la FIFA kwa ngazi ya
vilabu.
Pamoja na TP Mazembe kushindwa katika michuano
ya kombe la shirikisho la CAF lakini bado Katumbi anasema anajiandaa
vyema na msimu ujao na mashindano mengine."Malengo yetu ni kuleta
ushindani mkubwa na ninaamini tunaweza kufikia mafanikio kwa kile
tulichonacho sasa"alisema Katumbi.
Katumbi pia ameiambia BBC kuwa iwapo
wataimarisha zaidi timu yao na kwamba haoni ni kwanini siku moja TP
Mazembe siku moja wasishinde kombe la dunia.
Mwaka 2010, timu hiyo ya soka ya Mazembe ndio
iliyokuwa klabu ya kwanza toka bara la Afrika kutinga fainali katika
mashindano ya kombe la dunia la FIFA kwa ngazi ya vilabu lakini
wakaondolewa na klabu ya Inter Millan ya Italia.
Baada ya michuano hiyo ya michuano hiyo ya
shirikisho timu hiyo toka mji wa Lubumbashi nchini Demokrasia ya Congo
wanatarajiwa kurejea tena katika michuano ya ligi ya mabingwa mwaka
ujao.
Tambo hizi za Mazembe ni kutokana na vipaji vya
kutosha kutoka katika shule ya vipaji vya michezo ambapo wanatarajia
baada ya miaka mitatu wantakuwa na wachezaji wenye uwezo wa kuwafikisha
na kushinda kombe la dunia.
Hata hivyo Katumbi kiongozi wa miongoni mwa timu
tajiri barani Afrika amesema kuwa ameweza kuhakikisha fedha
zinapatikana ili kuimarisha kikosi chake,kutengezeza uwanja mpya na wa
kisasa ikiwa ni pamoja na ununuzi wa ndege ya timu.
Mipango yake katika kupata wachezaji wa
kimataifa inaendelea ambapo kwa sasa anawachezaji nchi za nje ambapo kwa
ana wachezaji kutoka nchi za Tanzania, Ghana, Zambia, Cameroon,
Botswana na hivi karibuni amesajili kutoka Malawi.
Timu hii ya TP Mazembe ni miongoni mwa timu
ambazo wachezaji wake wanalipwa vizuri kwa viwango vya Afrika ikiwa ni
jitihada za Katumbi kupunguza kaksi ya vipaji vya Afrika kupotelea
ulaya.
"Wachezaji wazuri wa Afrika wanakwenda ulaya kwa
sababu ya malipo mazuri kutokana na kutolipwa vizuri hapa Afrika"
anasema Katumbi.
Katumbi anasema kuwa sera yao ni kuwachukua
wachezaji toka nchi za Afrika ili kuonyesha umoja ndania ya bara hilo na
kwamba Afrika ni nnzuri lakini kinachotakiwa ni umoja hasa kutokana na
mapigano ambayo yamekuwa yakitokea kila siku katika bara la Afrika.
No comments:
Post a Comment