KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, January 15, 2014

Fainali za CHAN: Uganda Cranes kuamua hatma yao ya hatua ya mtoano kesho dhidi ya Zimbabwe


Timu ya taifa ya Uganda (Uganda Cranes) inamatumaini makubwa ya kuweka vizuri nafasi yao ya kutinga katika hatua ya mtoano ya fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN ambapo watakuwa wa kibarua cha kukabiliana dhidi ya  Zimbabwe katika uwanja wa Athlone hapo kesho mchana ukiwa ni mchezo wa kundi B.
Uganda ilianza michuano hiyo kwa matokeo mazuri baada ya kuwachapa Burkina Faso walioshiriki kwa mara ya kwanza kwa mabao.
 The Cranes wanaongoza kundi hilo wakiwa na alama 3 ikiwa ni alama mbili mbele ya wanaowafuatia. Ni timu pekee kutoka kundi hilo la B kupata alama zote tatu mpaka sasa.

Uganda ilikuwa ni timu ambayo haikupewa nafasi na mashabiki wa soka kama itafanya vema kabla ya kuanza kwa fainali hizo, huku kigogo cha Afrika Morocco na washindi wa pili wa fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2013 Burkina Faso wakitarajiwa kuwa tishio katika kundi hilo na pengine wangekuwa na upinzani kidogo kutoka kwa Zimbabwe.
Licha ya kuongoza kundi, kocha wa kikosi hicho Milutan Sredojevic bado anadhani kikosi chake ni 'underdogs' katika kundi hilo na michuano hiyo kwa ujumla.
Kocha huyo wa zamani wa Orlando Pirates anadhani kikosi chake si imara kwakuwa kimekuwa na uzoefu mdogo katika medani ya kimataifa.
 “Tusubiri mpaka mchezo wa pili hapo ndipo tutakapo ona kama bado ni 'underdogs'”
Baada ya sare dhidi ya Morocco katika mchezo wa kwanza Zimbabwe inatarajiwa kuwa na hali ya kujiamini zaidi kuelekea kwenye mchezo huo wa kesho dhidi ya Uganda.

No comments:

Post a Comment