Aston Villa wamemchukua straika Grant Holt kwa mkopo kutoka kwa
Wigan Athletic kwa kipindi cha msimu kilichosalia.
Klabu hiyo inayoshiriki Ligi ya
Premia imesema hayo kupitia tovuti yake ya klabu.
Holt, ambaye alijiunga na mabingwa wa sasa wa Kombe la FA Wigan mwaka
uliopita akitokea Norwich City, amejiunga tena na meneja wake wa zamani
Paul Lambert.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye alifunga mabao 53 katika
mechi 92 alizochezea Norwich, amechukuliwa na Villa kujaza pengo
lililoachwa na Libor Kozak ambaye ni majeruhi.
"Kumpoteza Libor kutokana na jeraha ni pigo kwetu, bila shaka.
Nilipojua kwamba Grant alikuwa amewekwa sokoni nilitaka haraka kumchukua
kwa sababu ataongeza nguvu na uzoefu katika kikosi chetu ambacho kwa
jumla bado kinahitaji mabadiliko” Lambert aliambia avfc.co.uk.
"Ninajua yale anaweza kufanya na hilo ni muhimu.”
Villa wako nambari 11 katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza, alama
tano kutoka eneo la kushushwa ngazi na wametatizika katika kufunga mabao
msimu huu. Wamefunga mabao manane pekee nyumbani msimu huu.
"Kuweza kurudi tena katika Ligi ya Premia, hasa katika klabu kubwa
kama Villa, ni jambo kubwa kwangu na fursa kwangu kufanya kazi tena na
meneja wangu wa zamani na watu wake," Holt alisema.
"Sote tunafahamu kwamba hii ni klabu iliyo katika mpito lakini
tunapiga hatua. Tuna vijana wengi wachanga kwenye klabu ambao wanafanya
kazi nzuri na nina furaha kujiunga nao na kuweza kusaidia,” akaongeza.
No comments:
Post a Comment