KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, January 15, 2014

Manchester United wazodoka katika harakati za kumnasa mlinzi wa Everton Leighton Baine

Leighton Baines anakaribia kukubali mpango mwingine wa muda mrefu wa kusalia katika klabu yake ya Everton.
Meneja wa zamani wa Toffees David Moyes mara mbili amekwaa kisiki katika jaribio lake la kutaka kumsajili mlinzi huyo wa kushoto wa kimataifa wa wa England mwenye umri wa miaka 29 ili ajiunge nao Manchester United.
Everton sasa inajiongezea hali ya kujiamini zaidi kuwa watafanikisha mpango huo kwa Baines, ambaye alijiunga nao akitokea klabu ya Wigan kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 6 Agosti 2007 na ameendelea kuwa katika kiwango cha juu katika kipindi chote hicho.

Inafikiriwa kuwa mpango huo utagharimu mshahara wa wa pauni £75,000 kwa wiki.
Baada ya kushindwa mpango wa kumchukua mara mbili ikiwa ni pamoja na mpango wa Baines kuelekea Old Trafford sambamba na kiungo Marouane Fellaini kwa ada ya uhamisho ya kujumlisha yenye thamani ya pauni £28m na taarifa zinasema Manchester United sasa wanaonekana kusaka mlinzi wa pembeni wa kushambulia 'attacking full-back'.
Lakini inavyoonekana kwa sasa ni kama Moyes yuko kwenye mpango wa kuishawishi  Southampton kwa ajili ya Luke Shaw na Fabio Coentrao wa Real Madrid naye yuko katika rada ya klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment