Karl-Heinz Rummenigge amekuwa mtu wa kwanza mashuhuri (high profile official) kulitaka shirikisho la soka Ulaya kuitumia sheria yake ya 'Financial Fair Play' akisema lazima itumike dhidi ya Paris St Germain endapo watavunja utaratibu.
Sheria hiyo maarufu kama FFP ambayo imeaanza rasmi kutumika baada ya kuwepo kwa kipindi kirefu cha mpito cha takribani miaka mitatu, inataka vilabu visitumie pesa nyingi kuliko wanavyo ingiza kupitia haki zao za TV, mapato ya milangoni , udhamini na pesa za kushindania mataji.
Utaratibu wa eufa unaruhusu kuwepo kwa madeni ndani ya vilabu lakini umetengezwa kukataza matumizi makubwa katika mishahara mikubwa pamoja na uhamisho wa ada ya kupindukia kutoka kwa wamiliki wenye fedha nyungi yaani 'mataikun'.
"Sidhani kama ni sawa kwa Paris St Germain wanaweza kupingana Financial
Fair Play," amenukuliwa mwenyekiti huyo wa mabingwa wa Ulaya Bayern Munich
ambaye pia ni mwenyekiti wa umoja wa vilabu ulaya (European Club Association) alipokuwa akiongea katika kongamano la 'SpoBis business' kule Duesseldorf nchini Ujerumani hii leo.
PSG inayomilikiwa na Qatar Investment Authority, haikuweza kupatikana kutoa maoni juu ya hilo.
Wiki iliyopita meneja wa Chelsea Jose Mourinho, ambaye klabu yake inamilikiwa na tajiri Tycoon wa Urusi Roman Abramovich, aliweka tahadhari juu ya matumiza ya makubwa ya klabu ya Manchester
City, ambayo inamilikiwa na bilionea Sheikh Mansour Bin Zayed Al Nahyan of
Abu Dhabi.
Habari kutoka nchini Uingereza zinaarifu kuwa wanasheria wanajaribu kukabiliana na haki dhidi ya City endapo itafanikiwa kutinga michuano ya vilabu barani Ulaya msimu ujao.
Wapinzani wa Manchester City wanaitaka wanajaribu kushinikiza kuwepo na matumizi ambayo yatakwenda sawia na mahitaji ya sheria hiyo ya Uefa.
No comments:
Post a Comment