Klabu cha ligi ya Premier, Fulham, walizidi kufedheheshwa pale
walipongolewa kutoka kombe la FA na Sheffield United wanaocheza daraja
ya tatu Uingereza.
Washikilia mkia hao wa Premier walichakazwa 1-0 nyumbani kwao Craven Cottage kwenye mechi iliyolowa kutokana na mvua kali.
Kivumbi hicho kilielekea kuamuliwa na mikwaju ya penalti baada ya
ukosefu wa nafasi wazi za kufunga na kuzembea kwa mashambulizi hadi
Shaun Miller alipoibuka nyota dakika ya 120.
Miller alitia kizimbani kupitia kichwa baada ya kunganishiwa na
mwenzake Harry Maguire huku United wakiongeza Fulham kwa kaburi lao la
timu za Premier baada ya kuondoa Aston Villa katika raundi ya tatu ya
kombe hilo.
United wanajiandaa kuchuana na Preston North End au Nottingham
Forest katika raundi ya tano huku Fulham, walioanguka hadi nafasi ya
mkia katika Premier baada ya kushindwa mechi nne mtawalia wakikondolea
masaibu.
No comments:
Post a Comment