Mchezaji wa Bayer Leverkusen Sydney Sam akiugulia maumivu |
Katika kinyang'anyiro cha kombe la shirikisho , DFB Pokal, timu nne
zimefanikiwa kuingia duru ya nusu fainali. Timu hizo ni Borussia
Dortmund, Bayern Munich, Kaiserslautern na Wolfsburg.
Jana timu ya daraja la pili ya Kaiserslautern iliiondoa Bayer Leverkusen
katika kinyang'anyiro cha kombe la shirikisho la Ujerumani DFB Pokal
katika mchezo wa robo fainali, baada ya kushinda kwa bao 1-0 katika
mchezo ambao ulichezwa kwa muda wa dakika 120 baada ya timu hizo kutoka
sare bila kufungana katika muda wa kawaida.
Wolfsburg iliishinda nguvu Hoffenheim kwa mabao 3-2 na Bayern Munich ilidhihirisha ubabe wake kwa kuishinda Hamburg kwa mabao 5-0.
Timu nne Wolfsburg, Kaiserslautern, na Bayern Munich zimeingia nusu fainali ambapo Borussia Dortmund ilikuwa timu ya kwanza kukata tikiti yake kwa kuishinda Eintracht Frankfurt kwa bao 1-0 siku ya Jumanne.

No comments:
Post a Comment