Winga wa Bayern Munich, Franck Ribery, hataweza kurejea uwanjani hadi
angalau mwezi Machi akiwa anauguza kidonda chake baada ya kufanyiwa
operesheni ya makalio.
Gazeti la kila siku nchini Ujerumani, Bild, limesema
mwanamichezo huyo mwenye umri wa miaka 30 anatazamiwa kukosa mechi tatu
za Bayern baada ya operesheni ya hapo Alhamisi kurekebisha mshipa mmoja
wa damu uliopasuka.
Huku Bayern ikiongoza ligi ya Ujerumani kwa pointi 13, Ribery atakosa
mechi mbili za Bundesliga na pia mechi ya Jumatano ya Lgi ya Mabingwa,
Champions League, ambapo timu yake itacheza mchezo wake wa kwanza na
Arsenal.
Ribery hatarajiwi kurejea uwanjani hadi wakati mechi ya nyumbani dhidi
ya Schalke 04 tarehe 1 Machi, endapo tu jeraha lake litakuwa limepona.
Ikiwa jeraha hilo litaleta mashaka yoyote, basi Ribery anaweza kujikuta
amechelewa kwa matayarisho ya raundi ya pili ya mechi ya Ligi ya
Mabingwa dhidi ya timu ya Uingereza maarufu pia kama Gunners tarehe 11
Machi.
Mchezaji huyo mwenye asili ya Kifaransa anatazamiwa kuanza mazoezi
madogo madogo mwishoni mwa wiki hii, kuanza kukimbia wiki moja baadaye.
No comments:
Post a Comment